Tuesday, June 19, 2012

ASKARI WALIOHUSIKA NA MAUAJI YA ALIYEKUWA MSANIFU MAJENGO NA MCHORA RAMANI ARUSHA WAACHIWA HURU..


ASKARI wawili waliodaiwa kuhusika na mauaji ya aliyekuwa msanifu wa majengo na mchora ramani wa manispaa ya Arusha, Mussa msofe, wameachiwa huru, baada ya Mahakama Kuu kanda ya moshi kutomkuta na hatia mshtakiwa wa kwanza na Mkurugenzi wa mshtaka nchini DPP, kuondoa mashtaka shidi ya mshtakiwa wa pili.

Awali wakili wa serikali, osca ngole, aliieleza mahakama hiyo kuwa dpp, chini ya kifungu namba 91 910 cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai sura ya 20, ambacho kinampa mamlaka kumfutia mashtaka mshtakiwa yoyote, ameondoa mashtaka dhidi ya Ex 1089 pc isaya.
Aidha, baada ya taarifa hiyo, wakili huyo alisoma maelezo ya awali ya kesi ya kuua bila kukusudia inayomkabili mshtakiwa kwa kwanza , Ex 7027, Pc James Marwa, ambaye alikiri kutenda kosa hilo, ambapo katika maelezo hayo ilielezwa kuwa tukio la mauaji hayo lilitokea Januari 23, mwaka 2004 katika eneo la makutano ya barabara ya KIA.

Alidai kuwa marehemu alitokea mkoani Arusha na kufika kwenye eneo hilo katika baa ya Rose, ambapo polisi wane walifika baada ya muda mfupio na kuuliza mwenye gari lakini hakujitokeza hadi walipochukua uamuzi wa kulifunga gari lake na ndipo alipojitokeza akiwa na sime.

Alidai palitokea kurupushani baina yao na ndipo marehemu alipokimbilia ndani na kujifungia kwenye moja ya vyumba vyenye mlango wa grili, na kutishia kuua yoyote atakayemsogelea, na ndipo askari hao walipoomba msaada kwa aliyekuwa mkuu wa kituo cha polisi cha kia,saimon haule, kwa madai kuwa kuna jambazi wanapambana nalo ambaye alifika akiwa na askari wengine akiwemo mshtakiwa wa kwanza, alimsihi marehemu kufungua mlango na kumuhakikishia usalama wake alkini alikataa.

Ngole alidai askari hao walipata ufunguo wa ziada na kisha kumpa mkuu huyo wa kituo ambaye alifungua bila marehemu kujua na askari walivamia ndani, na yalianza mapambano na katika mapambana hoyo ndipo risasi moja ilitoka kwenye bunduki aliyokuwa nayo mshtakiwa wa pili Pc isaya na kumpata marehemu eneo la tumbo na kufariki dunia muda mfupi kabla ya kufika hospitali ya mkoa wa kilimanjatro ya mawenzi.

Baada ya maelezo hayo, jaji mfawidhi wa mahakama hiyo, stella mugasha, alisema haoni haja ya kumtia hatiani mshatkiwa marwa kwa kuwa alikuwa katika harakjati za kumsaidia pc isaya na ndipo risasi ilifyatuka kwa bahati mbaya.

“Nimepitia maelezo ya mshtakiwa na mashahidi ambao wanapaswa kutoa ushahidi kwenye kesi hii, ambao ni mshala, honest na amini sijaona mahali ambako wanamtia hatiani mshatkiwa kwa kosa la kuua bila kukusudia na mshtakiwa hakuwepo kwenye tukio bali alikuja baadaye” alisema

Hata hivyo, baada ya kusomwa kwa maamuzi hayo, mke wa marehemu msofe, eling msofe, akizungumza na waandishi wa habari nje ya mahakama, alisema wanakusudia kukata rufaa kwenye mahakama ya rufaa kutokana na kutotrendewa haki.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment