Tuesday, May 22, 2012

KILIMANJARO TAILENTED YOURH SPORT CENTRE.(KITAYOSC)YAPATA YAZINDUA WEBSITE NA KUPATA WAALIMU WA MICHEZO KUTOKA HIGLANDS.

Baadhi ya wanafunzi wanaolelewa na kituo cha kukuza vipaji cha KITAYOSC wakionesha mbwembwe zao kwenye mechi iliyochezwa wakati walipotembelewa na wageni kutoka Highlands pamoja na kuzindua website ya kituo hicho
                                                                                    
wanafunzi wasichana wanaolelewa na kituo cha kukuza vipaji cha KITAYOSC wakionesha mbwembwe zao kwenye mechi iliyochezwa wakati walipotembelewa na wageni kutoka Highlands pamoja na kuzindua website ya kituo hicho
    
Bernard Mnyeyelwa afisa elimu taalumu idara ya elimu ya sekondari manispaa ya Moshi ambaye alikuwa mgeni rasmi akizungumza kwenye tamasha hilo la uzinduzi wa website pamoja na kupokea wageni wataofunsisha michezo kutoka Highlands

Wageni kutoka highlands ambao ni ma coarch wanasoma chuo kikuuu cha highlands wakicheza mchezo yao ya asili huko Highlands ambao wanatumia magongo.

Michezo mbalimbali ilikuwepo ikiwemo kuvuta kamba ambapo wageni waliburuzwa,

Wageni kutoka Highlands walikuwa na zawadi mbalimbali ikiwemo jezi pamoja na mipira kwa ajili ya watoto hao ambao wananolewa na kituo hicho.


Katika jitihada za kuweza kukuza soko la miguu nchini imeelezwa kuwa wananchi na viongozi wanatakiwa kuamka na kkunga mkono jitihada za wadau mbalimbali hususani ni wale ambao wamekuwa wakijihusisha na kuibua na kuendeleza vipaji.
Hayo yalizungumza na Afisa Elimu taaluma kitengo cha elimu ya Sekondari Manispaa ya Manispaa ya Moshi, Bernard Mnyeyelwa ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa mtandao yaani website ya kituo cha kulea na kukuza vipaji cha(KITAYOSC) inayoenda kwa jina la www.kilimanjarotalents.com.
Alisema kuwa Mkoa wa Kilimanjaro ni moja ya mikoa ambayo ilikuwa ikifanya vizuri kwenye mpira wa miguu lakini kwa sasa hali imekuwa tofauti,ambapo amesema kuwa uzinduzi wa mtandao huo pamoja na  mchango unaotolewa na kituo hicho utasaidia kunyanyua mpira wa miguu mkoani hapa.
“Hata Manispaa ina mipango mbalimbali kwenye mambo ya mpira wa miguu kama  kutafutwa mzabuni kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu uliopo eneo King George Memorial kwa ajili ya kuendelea kuendeleza mpira wa miguu”Alisema Bernard.
Kwa upande wake Meneja  Mipango Godfrey Madengwa  wa kituo cha KITAYOSC alisema kuwa uzinduizi wa website hiyo utasaidia kutangaza kituo hicho kazi ambazo zimekuwa zikifanya pamoja na kuweka malengo ya kituo hicho walipotoka na walipofikia hadi sasa.
Alisema kuwa mbali na uzinduzi wa mtandao huo lakini pia wamepokea wageni kutoka Highlands ambao ni wanafunzi ma coarch ambao watakuwa kituoni hapo kwa ajili ya kuwanoa watoto hao ambao wana umri wa miaka 15 kushuka chini lengo likiwa ni kuibua na kuendeleza vipaji.

Hata hivyo katika wakati mwingine alisema kuwa kituo hicho kimekuwa kikichukua pia watoto wanaoishi katika mazingira magumu pamoja na kuwajenga watoto kisaikolojia na kueweza kuepukana na vishawishi kama kujiingiza kwenye ngono na kufikiria michezo.

1 comment:

  1. EXAUD JOHN MAKYAO
    WA - JIMBO LA VUNJO MOSHI.
    makyaoexaud@yahoo.com.

    NATOA PONGEZI ZA THAT KWA KUANZISHWA KWA KITUO HIKI (KITAYOSC).

    MAWAZO YA KUANZISHA KITUO KAMA HIKI YATAKUBALIWA NA KILA MTANZANIA MPENDA MAENDELEO.

    TUMEKOSA FURSA NYINGI KIMICHEZO KWASABABU YA KUKOSEKANA VITUO KAMA HIVI.

    NIKO PAMOJA NANYI KATIKA KUTETEA UMUHIMU WA KUIBUA NA KUKUZA VIPAJI VYA WATANZANIA WA SASA NA VIZAZI VIJAVYO.

    I promise to visit this centre when I get chance.Kindly keep it up.

    ReplyDelete