KILIMANJARO TAILENTED YOURH SPORT CENTRE.(KITAYOSC)YAPATA
YAZINDUA WEBSITE NA KUPATA WAALIMU WA MICHEZO KUTOKA HIGLANDS.
Bernard Mnyeyelwa afisa elimu taalumu idara ya elimu ya sekondari manispaa ya Moshi ambaye alikuwa mgeni rasmi akizungumza kwenye tamasha hilo la uzinduzi wa website pamoja na kupokea wageni wataofunsisha michezo kutoka Highlands |
Wageni kutoka highlands ambao ni ma coarch wanasoma chuo kikuuu cha highlands wakicheza mchezo yao ya asili huko Highlands ambao wanatumia magongo. |
Michezo mbalimbali ilikuwepo ikiwemo kuvuta kamba ambapo wageni waliburuzwa, |
Wageni kutoka Highlands walikuwa na zawadi mbalimbali ikiwemo jezi pamoja na mipira kwa ajili ya watoto hao ambao wananolewa na kituo hicho. |
Katika jitihada za kuweza kukuza soko la miguu nchini
imeelezwa kuwa wananchi na viongozi wanatakiwa kuamka na kkunga mkono jitihada
za wadau mbalimbali hususani ni wale ambao wamekuwa wakijihusisha na kuibua na
kuendeleza vipaji.
Hayo yalizungumza na Afisa Elimu taaluma kitengo cha elimu
ya Sekondari Manispaa ya Manispaa ya Moshi, Bernard Mnyeyelwa
ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa mtandao yaani website ya kituo
cha kulea na kukuza vipaji cha(KITAYOSC) inayoenda kwa jina la www.kilimanjarotalents.com.
Alisema kuwa Mkoa wa Kilimanjaro ni moja ya mikoa ambayo
ilikuwa ikifanya vizuri kwenye mpira wa miguu lakini kwa sasa hali imekuwa
tofauti,ambapo amesema kuwa uzinduzi wa mtandao huo pamoja na mchango unaotolewa na kituo hicho utasaidia
kunyanyua mpira wa miguu mkoani hapa.
“Hata Manispaa ina mipango mbalimbali kwenye mambo ya mpira
wa miguu kama kutafutwa mzabuni kwa
ajili ya ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu uliopo eneo King George Memorial
kwa ajili ya kuendelea kuendeleza mpira wa miguu”Alisema Bernard.
Kwa upande wake Meneja Mipango Godfrey Madengwa wa kituo cha KITAYOSC alisema kuwa uzinduizi
wa website hiyo utasaidia kutangaza kituo hicho kazi ambazo zimekuwa zikifanya
pamoja na kuweka malengo ya kituo hicho walipotoka na walipofikia hadi sasa.
Alisema kuwa mbali na uzinduzi wa mtandao huo lakini pia
wamepokea wageni kutoka Highlands ambao ni wanafunzi ma coarch ambao watakuwa
kituoni hapo kwa ajili ya kuwanoa watoto hao ambao wana umri wa miaka 15
kushuka chini lengo likiwa ni kuibua na kuendeleza vipaji.
Hata hivyo katika wakati mwingine alisema kuwa kituo hicho
kimekuwa kikichukua pia watoto wanaoishi katika mazingira magumu pamoja na
kuwajenga watoto kisaikolojia na kueweza kuepukana na vishawishi kama
kujiingiza kwenye ngono na kufikiria michezo.
EXAUD JOHN MAKYAO
ReplyDeleteWA - JIMBO LA VUNJO MOSHI.
makyaoexaud@yahoo.com.
NATOA PONGEZI ZA THAT KWA KUANZISHWA KWA KITUO HIKI (KITAYOSC).
MAWAZO YA KUANZISHA KITUO KAMA HIKI YATAKUBALIWA NA KILA MTANZANIA MPENDA MAENDELEO.
TUMEKOSA FURSA NYINGI KIMICHEZO KWASABABU YA KUKOSEKANA VITUO KAMA HIVI.
NIKO PAMOJA NANYI KATIKA KUTETEA UMUHIMU WA KUIBUA NA KUKUZA VIPAJI VYA WATANZANIA WA SASA NA VIZAZI VIJAVYO.
I promise to visit this centre when I get chance.Kindly keep it up.