MKUU WA MKOA WA KAGERA ATOA SOMO KWA WAANDISHI.
![]() |
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe akiwaonyesha waandishi wa habari baadhi ya habari zilizochapishwa katika magazeti hivi karibuni zinazohusu Mkoa wa Kagera |
![]() |
Waandishi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa. |
MKUU wa Mkoa wa Kagera
Kanali Mstaafu Fabian Massawe amewaasa waandishi wa habari Mkoani hapa
kutoa kipaumbele kwa habari za kutangaza maendeleo na fursa mbalimbali
zilizopo.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo mchana Kanali Massawe amesema habari nyingi za maendeleo hazijatangazwa vya kutosha katika vyombo vingi vya habari kama ilivyo katika Mikoa mingine.
Amesema Mkoa wa Kagera unatekeleza mipango mingi ya maendeleo ambayo haipewi nafasi kubwa na waandishi wa habari na kuwataka pia kuandika habari za kuvutia fursa mbalimbali za uwekezaji.
'Mkoa wetu wa Kagera una ukame wa habari katika vyombo vingi vya habari,tunataka uanze kusikika tangazeni pia mambo yanayoweza kuwaathiri wananchi ili mradi mpate ufafanuzi wa viongozi husika'alisema Massawe
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa aliwakumbusha waandishi wa habari kwenda kwa viongozi sahihi wanaoweza kutoa ufafanuzi wa habari au mambo wanayoyafuatilia kabla ya kuyatangaza au kuchapishwa katika vyombo vya habari.
Alitumia nafasi hiyo ya kusisitiza kampeini ya usafi inayoendelea katika Wilaya zote za Mkoa wa Kagera huku akiwataka wananchi kutoa ushirikiano kuwabaini watu wanaowaachisha wanafunzi wa kike masomo baada ya kuwabebesha ujauzito.
Pia Massawe aliwaonya viongozi wa kisiasa wanaokwamisha utekelezaji wa mambo mbalimbali katika maeneo yao kwa kisingiziio cha kuwatetea wapiga kura wao.

habari na gordon kalulunga..kalulunga press network tz.
Thanks for providing such a great article, it was excellent and very informative. as a first time visitor to your blog I am very impressed. I found a lot of informative stuff in your article. Keep it up. Thank you.
ReplyDeletesunflower lecithin