ZAO LA TUMBAKU KAHAMA LAENDELEA KUSHIKA KASI...
![]() |
| Mkulima wa Tumbaku akiwa shambani zao ambalo linadaiwa kupita mapato ya madini kwa sasa |
![]() |
| PICHA YA ENEO LA MGODI WA BULYANHULU KAKOLA |
HALMASHAURI ya Wilaya ya Kahama
imepitisha mpango wa bajeti ya sh bilioni 43.7 kwa mwaka 2012/2013 huku
katika mapato yake ya ndani yanayotarajiwa kuongezeka kwa asilimia
27.6 yakiongozwa na zao la tumbaku
Hali hiyo inadhihirisha wazi kuwa mapato
hayo yanapiku yale ya migodi miwili ya dhahabu ya Bulyanhulu na Buzwagi
inayomilikiwa na Kampuni ya African Barrick Gold Mine.
Katika
bajeti ya mwaka huu, halmashauri hiyo, inatarajia kutumia kiasi hicho
cha fedha ikiwa ni ongezeko la asilimia 1.5 kutoka bajeti iliyopita kwa
ajili ya matumizi ya kawaida, mishahara sambamba na miradi mbalimbali
ya maendeleo.
Katika bajeti iliyopita hadi kufikia
Machi mwaka huu, sh 13.6 sawa na asilimia 31.5 kati ya sh milioni 43.1
zilizopitishwa ndizo zimekusanywa.
Kwa mujibu wa Ofisa Mipango wa
halmashauri hiyo, Duncan Thebas, fedha hizo ni pamoja na sh bilioni 4.9
kutoka vyanzo vya mapato ya ndani, ikiwemo migodi ya dhahabu ya
Bulyanhulu na Buzwagi pamoja na makampuni ya kununua zao la tumbaku.
Aidha, katika taarifa hiyo, alisema kuwa
migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu itachangia jumla ya dola za Marekani
laki nne sawa na wastani wa sh milioni 600 huku makampuni ya kununua zao
la tumbaku yakilipia ushuru wa sh milioni 720.
Kutokana na mpango huo wa bajeti, zao la tumbaku ndilo
linaloongoza kuchangia kwa kiasi kikubwa katika mapato ya ndani katika
Halmashauri ya Wilaya ya Kahama tofauti na jamii inavyodhani kuwa
dhahabu ndiyo inayochangia mapato makubwa,



No comments:
Post a Comment