Mbunge wa jimbo la Ludewa mkoani Njombe Deo Filikunjombe jioni hii
ameiweka serikali ya Rais Jakaya Kikwete njiapanda baada ya
kueleza ya moyoni kuwa mawaziri wa JK ni wezi na ana ushahidi wa
kutosha hali iliyoonyesha wazi kuchafua hali ya hewa bungeni jioni
ya leo . Hii ni mara ya pili kwa mbunge Filikunjombe kueleza ya
moyoni ambapo safari ya kwanza alipata kusema bungeni kuwa mawaziri
wanaokwamisha serikali ni vema wakanyongwa kuliko wananchi wa
Ludewa kuendelea kufa maji ziwa nyasa kwa uzembe wa mawaziri hao |
No comments:
Post a Comment