Sunday, March 18, 2012

MSITU WA WEST KILIMANJARO UNAVYOSHIRIKANA NA WANANCHI KATIKA KUTUNZA MAZINGIRA NA WANANCHI KUJIPATIA KIPATO
Wakulima waliolima viazi katika eneo la Msitu wa West Kilimanjaro wakivuna mazao yao aina ya viazi


Uchumi wa eneo la West Kilimanjaro Wilatani Siha umekuwa kutokana na mazao yanayolimwa karibia mwaka mzima yakiwemo viazi na Caroti ambazo wakulima hujipatia vipato
Meneja wa Msitu wa West Kilimanjaro Bakari Mohamedi wakati akizungumza na blog ya Tanzania Leo.inayoonekana ni miche ya miti.


 Kuwepo kwa ushirikiano mzuri baina ya uongozi wa msitu wa West Kilimanjaro na wananchi wanaouzunguka msitu huo umesaidia kuendelea kuboresha msitu huo pamoja na wananchi kujipatia kipato.

Blog hii ya tanzania leo akiongea na meneja wa msitu huo Bakari Mohamedi  alisema kuwa wamejiwekea mazingira mazuri na mahusiano kwa wananchi kwa lengo la kuwatumia wananchi kuulinda msitu kama mali yao.
 Alisema Wananchi 15,000 kutoka Wilaya mbalimbali za Mkoa wa Kilimanjaro wananufaika na kilimo cha mazao mmbalimbali kwa nyakati tofauti katika msitu wa West Kilimanjaro Uliopo Wilayani Siha.
Alisema kuwa wananchi kutoka katika Wilaya za Rombo,Hai,Siha,na maeneo mengine hupata fursa ya kulima mazao kama viazi,mbogamboga,karoti mahindi maharage baada ya misitu kuvunwa.
Pia wakulima zaidi ya 7000 huweza kuingia kila siku kwenye msitu wa huo na kuweza kujipatia riziki kwa kufanya kazi mbalimbali ndani ya msitu,ikiweno wanaonunua,wanaosafirisha mazao yanayolimwa ndani ya Msitu.
Bakari alisema kuwa wakulima wanaogaiwa sehemu kwa ajili ya kilimo huweza kulima kwa muda wa miaka 5 na hivyo kuweza kujipatia kipato.
Alisema kuwa ugawaji wa maeneo kwa wananchi kwa ajili ya kilmo huzingatia pia makundi maalumu katika jamii hususani wasiojiweza na wanaoishi na virusi vua UKIMWI ili kuweza kujipatia riziki.
Aliongeza kuwa ushirikiano huo mzuri umekuwa ukisaidia kwa uongozi wa msitu kupata taarifa kwa baadhi ya wananchi ambao wamekuwa wakijaribu kuharibu mazingira pamoja na kuvamia msitu.
“Wananchi ambao tumekuwa tukiwapatia  maeneo kwa ajili ya kilimo wamekuwa wakitusaidia kupambana na watu ambao wanaharibu msitu pamoja na kuzuia upikaji wa gongo ndani yam situ”Alisema Bakari.
Mbali na hayo pia alisema ushirikishwaji huo wa wananchi umekuwa ukipunguza idara yam situ garama za usafishaji wa msitu baada ya uvunaji pamoja na upaliliaji wa wa miti baada ya kupandwa.


 
                                      Picha habari na Rodrick Mushi wa Blog ya tanzania leo

No comments:

Post a Comment