Sunday, June 17, 2012


WANANCHI WATAABIKA IPIMAJI WA MALARIA SAME
MKUU WA WILAYA SAME.
                                                                

WANANCHI wa kijiji cha Kizungo kata ya Vumari katika wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro wanatembea umbali wa hadi 20km kufika katika hospitali ya wilaya hiyo kwa ajili ya kupima vimelea vya ugonjwa wa malaria licha ya kuwepo kwa darubini katika zahanati ya kijiji.

Darubini ambayo haitumiki kwa zaidi ya miaka mitano tangu kununuliwa, kutokana na kukosekana kwa mtaalamu, ilinunuliwa na kutolewa kwa wananchi hao na mbunge wa Jimbo la Same Magharibi, Dr David Matayo kwa ajili ya kuwapunguzia wananchi hao adha ya kufuata huduma hiyo umbali mrefu.


Hatahivyo darubini hiyo tangu ikabidhiwe kwa kijiji hicho imehifadhiwa katika zahanati ya Kijiji hai wakati huu, huku wananchi wakiendelea kutaabika.


Mwenyekiti wa kijiji hicho, Kabaka Mndeme aliwaambia waandishi wa habari kijijini hapo juzi kuwa kukosekana kwa huduma hiyo wakati kifaa kinachohitajika kipo ni hatua ya makusudi kwa serikali kuwaataabisha kutafuta huduma hiyo mbali na kijiji chao.


Mndeme alisema wananchi wa kijiji hicho wanaiomba halmashauri na serikali kwa ujumla wake kuwapatia mtaalamu wa kupima ugonjwa huo ili malengo ya mbunge wao wa kuwaletea huduma karibu iweze kufikiwa.


Akitaja changamoto nyingine za kijamii zinazokikabil kijiji hicho  aliseama ni pamoja na mindombinu mibovu ya barabara kutokana na barabara yao iliyomuhimu kiuchumi na kijamii ya Kizungo-Mgagao kutofanyiwa ukarabati hivyo kuathiri kabisa shughuli za kiuchumi katika eneo hilo.


Aliongeza kuwa kukosekana kwa mtaalamu huyo wa kutumia darubini kunaenda sambamba na kukosekana kwa wataamu wa kada ya elimu hasa katika shule za msingi za Dido na Mbono hali ambayo alisema kunaathiri kiwango cha elimu kwa watoto wao.

No comments:

Post a Comment