Friday, December 21, 2012

FAMILIA YA WALEMAVU WATANO YAOMBA MSAADA.


Watoto wa tano wa familia moja ambao ni walemavu wa viungo eneo la chome Wilayani Sama wakiwa kwenye picha ya pamoja.


Familia ya watoto watano wenye ulemavu Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro wameomba jamii kujitokeza kusaidia kutokana na  ulemavu wa viongo ambao umekuwa ukiwakabili kwa muda mrefu sasa, na kuwafanya kuishi katika hali ngumu kimaisha.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mama wa watoto hao,Nirenjigwa Joseph alisema kuwa ana watoto nane lakini kati yao watoto watano ni walemavu na mume wake  Amini Joseph alifariki tangu mwaka 1992 na baada ya hapo yeye ndo amekuwa akilelea familia hiyo.

Watoto hao ni Joseph  Amini( 38),Nafikahedi( 33) ,Wediel(30) Gadison (28) na Julius(25)wote ni walemavu wa viongo ambao wanatembea kwa kutambaa  na wanahitaji kuwa na muangalizi wakati wote kwa hakuna wanaloweza kufanya.

Watoto walizaliwa wakiwa wazima lakini tatizo likaanzia kwenye kutambaa wakashindwa kusimama na tulijaribu kupeleka hospitali na kuambiwa kuwa haitawezekana tena .

Kwa sasa ukiwaangalia watoto hao tayari wameshakuwa wakubwa kabisa na changamoto kubwa ni kwamba familia haiwezi kuwaacha kukaa pekee yao kwani wapo pia wakike na jamii pia imekuwa na makusudio mabaya kwa wale wenye imani potofu juu yao au wanaopewa maagizo ya imani za kishirikina.

“Baada ya mume wangu kufariki nilikuwa nailelea familia mwenyewe na nilikuwa najishughulisha na kilimo siku na kazi nyingine ya kufanya,lakini nashukuru Mungu pia wapo watu waliojitoa kwa moyo lakini bado mahitaji ya kuwatunza ni makubwa sana”Alisema mama huyo.

Mmoja watoto wa familia hiyo ambaye ni kati ya watoto watatu ambao hawana tatizo la ulemavu ambaye ni Mwalimu Chediel Amini (28)alisema kuwa wapo wafadhili ambao  wamejitokeza kuwasaidia lakini bado tatizo ni kubwa kwani nyumba aliyojenga bado inahitaji kumaliziwa.

Kikundi cha utukufu kwa Mungu kupitia kwa Mwenyekiti wake Samweli Njau  baada ya kutembelea familia hiyo walisema kuwa watasaidia kufunga huduma ya maji pamoja na tenki la kuhifadhia  maji ili kusaidia kuondoa tatizo la maji lilipo kwenye familia hiyo.

Baada ya kutembelea familia hiyo waliona kuwa jamii hiyo inahitaji kusaidiwa kwani wanapoishi walemavu hao hakuna kivuli na wamekuwa wakitambaa kwenye jua na kusumbuliwa na tatizo la funza hivyo kusaidia kuweka baraza kwenye nyumba hiyo,ambapo wanasema msaada wao hautaishia tu hapo bali wataendelea kuhamasisha na jamii nyingine.

Chediel alisema kuwa anaomba watu wenye mapenzi mema kuweza kujitokeza kusaidia familia hiyo kwa chochote watakachokuwa nacho ili kupunguza ugumu wa maisha ambao wamekuwa wakiishi kutokana na familia kutegemea kilimo kuwalea watoto hao.

Kwa mawasiliano  ya mmoja wa mtoto wa familia hiyo Chediel Amini ambaye ndiye aliyebeba jukumu la kusaidia ndugu zake wenye ulemavu, simu 0654118385.

No comments:

Post a Comment