Friday, March 9, 2012

MBUNGE WA HAI NA MWENYEKITI WA CHADEMA TAIFA FREEMAN MBOWE AKIWA KWENYE HARAMBEE YA UNUNUZI WA GARI LA KUTOLEA HUDUMA ZA NENO NA MUNGU KANISA LA KKKT USHARIKA WA SIHA MKOANI KILIMANJARO

Mbunge wa jimbo la Hai Freeman Mbowe  amechanga kiasi cha shilingi million 10 kwenye harambe iliyofanyika kwenye kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanznaia KKKT Dayosisi ya Kaskazini usharika wa Sanya juu kwa ajili ya kununulia gari la kutoa huduma za neno la Mungiu kwa kikundi cha Uamsho.

Akizungumza wakati wa harambee hiyo Mbowe alisema kuwa ifike mahali wananchi wasitoe nafasi kwa kazi za kibinadamu zikachafua kazi ya Mungu,ambapo alisema kuwa shida imewafanya watu wengi kutenda matendo yasiyompendeza Mungu kwa ajili ya kujitafutia kipato.

Alisema kuwa vitendo vya ushirikina vimekidhiri nchini,huku viongozi wakubwa wan Nchi wanaotegemewa kuongoza nchi wakitegemea kuongozwa na vitendo vya kishirikina,hususani wabunge wa jamhuri ya Muuungano ambapo wanategemea ushirikina kuweza kupata nafasi hizo za kuwawakilisha wananchi.

Mbowe ambae pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)Taifa alisema kuwa zaidi ya asilimia 80 ya wabunge wa Nch wanategemea vitendo vya kishirikina,na wengi wanatoka vyama mbali mbali vya siasa na ukikaa nao ndipo utaweza kugundua kwa matendo yao hususani na katika kuongoza na kuchaguliwa yanategemea nguvu za giza.

“Shida imewafanya wananchi kujiingiza katika vitendo viovu ikiwemo kuanzisha makanisa ili kujipatia vipato,viongozi wa dini tunawategemea sana,katika mambo mengi ya Nchi hii ikiwemo kusaidia kupatika kwa viongozi wanaoweza kuiongoza hii Nchi”Alisema Mbowe.

 Harambee hiyo ilihudhuriwa na vioongozi mbalimbali wakiwemo wale wa  dini wa siasa,ambapo kwa upande wa Mbunge wa Jimbo hilo Agrey Mwandry hakuwezi kufika,licha ya kualikwa na kutajwa jina lake wakati wa utambulisho wa wageni walioalikwa,bila ya kuwepo kwa muakilishi wake.

Miongoni mwa wanasiasa waliokuwemo kwenye harambee hiyo alikuwemo pia mgombea wa ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya Chadema Humpfrey Tuni ambae kura zake hazikutosha akichangia kiasi cha shil milioni moja kwa ajili ya ununuzi wa gari hilo.

Jumla ya zaidi ya shilingi mill 14  ziliwezeza kupatikana kwa ajili ya ununuzi wa gari hilo.ambapo lengo lilikuwa ni kupata kiasi cha shilingi million 50 katika kununua gari hilo la kutolea huduma za kiroho.


No comments:

Post a Comment