Waziri
wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe (mwenye miwani,) akikata utepe
kuashiria uzinduzi wa Mradi Mkubwa wa Maji Vijijini katika Kata ya
Endagile Babati Kijijini Jumatano wiki hii. Kulia kwa Mhe. Waziri ni
Mbunge wa Babati Vijijini Mhe. Jeetu Soni.
Waziri
wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe (mwenye miwani,) akifunua pazia
kuashiria uzinduzi wa Mradi Mkubwa wa Maji Vijijini katika Kata ya
Endagile Babati Kijijini Jumatano wiki hii. Kulia kwa Mhe. Waziri ni
Mbunge wa Babati Vijijini Mhe. Jeetu Soni.
Waziri
wa Maji Mhe. Prof. Jumanne Maghembe akimtishwa ndoo ya Maji Fatuma
Maulid baada ya kuzindua Mradi Mkubwa wa Maji Vijijini. Wa kwanza
kushoto ni Diwani wa Kata hiyo Mhe. Nicodemus Tarmo.
WAZIRI WA HABARI AFUNGUA KIKAO KAZI CHA SEKTA YA UTAMADUNI
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara
akifungua Kikao Kazi cha tisa cha Wadau wa Sekta ya Utamaduni nchini
(hawapo Pichani).Kikao hicho kilifanyika Jijini Dar es Salaam hivi
karibuni na kauli mbiu ilikuwa ni Urasimishaji wa tasnia za Filamu na
Muziki uwe Chachu ya Maendeleo. (Picha na Benjamin Sawe wa WHVUM).
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Sethi
Kamuhanda akisisitiza jambo kwa katika Kikao cha tisa cha wadau wa Sekta
ya Utamaduni kilichofanyika hivi karibuni Jijini Dar es Salaam. Kauli
mbiu ya Kikao hicho ni Urasimishaji wa tasnia za Filamu na Muziki uwe
chachu ya Maendeleo.Kushoto ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni
Profesa Hermas Mwansoko. (Picha na Benjamin Sawe wa WHVUM).
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akiteta
jambo na Katibu Mkuu Bw. Sethi Kamuhanda wakati wa Kikao cha tisa cha
wadau wa Sekta ya Utamaduni kilichofanyika hivi karibuni jijini Dar es
Salaam. (Picha na Benjamin Sawe wa WHVUM).
Kikundi
cha Wasanii wa ngoma za asili ambacho kikitumbuiza wakati wa ufunguzi
wa Kikao kazi cha tisa cha wadau wa Sekta ya Utamaduni kilichofanyika
hivi karibuni Jijini Dar es Salam. (Picha na Benjamin Sawe wa WHVUM).
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara
akimpongeza Mghani Mashairi Bwana Mohamed Lukemo wakati wa ufunguzi wa
Kikao kazi cha tisa cha Sekta ya Utamaduni kilichofanyika hivi karibuni
Jijini Dar es Salaa. (Picha na Benjamin Sawe wa WHVUM).
Wadau
wa Sekta ya Utamaduni nchini wakimsikiliza Wazari wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara (hayupo pichani) wakati wa
ufunguzi wa Kikao kazi cha tisa cha sekta hiyo kilichofanyika Jijini
Dar es Salaam hivi karibuni.Kauli mbiu ya Kikao hicho ni Urasimishaji wa
tasnia za Filamu na Muziki uwe chachu ya Maendeleo. (Picha na Benjamin
Sawe wa WHVUM).
ZIARA YA DK. SHEIN VIETNAM YAENDELEA SIKU YA PILI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
shein, akisalimiana na Makamo wa Rais Vietnam Bibi, Nguyen Thi
Doan,alipowasili Ikulu nchini Vietnam,akiwa na ujumbe wake katika ziara
rasmi ya Kiserikali nchini humo ya wiki moja.[Picha na Ramadhan Othman
Vietnam.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed shein, na Mkewe Mama Mwanamwema
Shein,wakipokea mashada ya mauwa kama ni Ishara ya ukaribisho katika
Ikulu ya Vietnam,alipofika kwa mazungumzo na Makamo wa Rais wa Vietnam
Bibi, Nguyen Thi Doan,akiwa na ujumbe wake katika ziara rasmi ya
Kiserikali nchini humo ya wiki moja.[Picha na Ramadhan Othman Vietnam.]
Mke
wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama
Mwamamwema Shein, akisalimiana na Makamo wa Rais wa Vietnam Bibi,
Nguyen Thi Doan,alipowasili Ikulu nchini Vietnam,alipofuatana na Rais wa
Zanzibar katika ziara Rasmi ya Kiserikali Nchini Vietnam ya wiki
moja.[Picha na Ramadhan Othman Vietnam.]
WATU WATATU WANAOSADIKIWA KUWA NI MAJAMBAZI WAUAWA MKOANI ARUSHA
Kamanda
wa polisi Mkoa wa Arusha kamishna Msaidizi wa Polisi Liberatus
Sabas akionyesha sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ0 ambazo
zilikutwa kwenye begi la watu watano ambao wanasadikiwa kuwa ni
majambazi .Tukio hilo lililtokea katika eneo la Olmatejoo jijini Arusha
leo asubuhi na Jeshi la Polisi lilifanikiwa kuwajeruhi kwa risasi Watatu
kati yao ambao baadae walifariki dunia wakiwa wanapelekwa hospitali .
(Picha na Mahmoud Ahmad Arusha)
………………………………………………………..
MNAMO TAREHE 22/11/2012 MUDA WA
SAA 3:45 ASUBUHI KATIKA ENEO LA OLMATEJOO HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA,
WATU WATATU (AMBAO MAJINA YAO BADO HAYAJATAMBULIKA) WANAOSADIKIWA
KUWA NI MAJAMBAZI WALIUAWA NA ASKARI WA JESHI LA POLISI WAKATI WA
WAJIBIZANO YA KURUSHIANA RISASI.
TUKIO HILO
LILITOKEA MARA BAADA YA JESHI LA POLISI MKOANI HAPA KUPATA TAARIFA
KUTOKA KWA RAIA WEMA AMBAO WALIELEZA KWAMBA, KATIKA ENEO HILO KULIKUWA
NA WATU WATANO AMBAO WANAWATILIA SHAKA, NDIPO BAADHI YA ASKARI
WALIKWENDA KATIKA ENEO HILO KWA AJILI YA KUFANYA UCHUNGUZI.
MARA BAADA YA ASKARI HAO KUFIKA
ENEO HILO, WATU HAO WALISHTUKA NA MMOJA WAO ALIYEKUWA NA SILAHA AINA YA
BASTOLA KIUNONI ALIITOA NA KUANZA KUWAFYATULIA RISASI ASKARI HAO.
KUTOKANA NA HALI HIYO ASKARI HAO WALIAMUA KUJIBU MAPIGO NA KUFANIKIWA
KUWAJERUHI WATU WATATU KATI YA WATANO NA WENGINE WAWILI WALIFANIKIWA
KUKIMBIA PAMOJA NA BASTOLA.
WATU HAO WALIFARIKI DUNIA WAKIWA
NJIANI WANAPELEKWA KATIKA HOSPITALI YA MOUNT MERU KWA AJILI YA MATIBABU.
ASKARI HAO WALIFANIKIWA KUPATA BEGI LILILOTUPWA NA WATU HAO NA MARA
BAADA YA KUPEKUA WALIKUTA BUNDUKI MBILI; MOJA AINA YA SHORTGUN NA
NYINGINE AINA YA RIFLE YENYE NO. 08805 AMBAYO ILIKUWA IMEKATWA MTUTU
PAMOJA NA KITAKO.
MBALI NA BUNDUKI HIZO PIA
WALIKUTWA NA RISASI 16 ZA SHORTGUN, KITAKO NA MTUTU WA BUNDUKI AINA YA
RIFLE, MTALIMBO (KIPANDE CHA CHUMA) AMBACHO KINASADIKIWA KUWA KINATUMIWA
KATIKA SHUGHULI ZA UVUNJAJI, RUNGU MOJA, PANGA MOJA, TUPA TATU ZA
KUNOLEA PANGA, SARE ZA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA (JWTZ) AMBAZO NI
SURUALI MOJA, T-SHIRT MOJA NA KOFIA MOJA. PIA ZILIPATIKANA KOFIA MBILI
ZINAZOTUMIKA KUFICHA USO PAMOJA NA KITAMBULISHO VYA KUPIGIA KURA,
LESENI YA UDEREVA NA KITAMBULISHO CHA MWANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI
DODOMA.
MPAKA HIVI SASA JESHI LA POLISI
MKOANI HAPA LINAENDELEA KUWATAFUTA WATU WAWILI AMBAO WALIKIMBIA NA PIA
LINAFANYA JITIHADA ZA KUWATAMBUA WATU WALIOUAWA AMBAPO MPAKA HIVI SASA
MIILI YAO IMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA MOUNT MERU. ASANTENI KWA
KUNISIKILIZA.
IMETOLEWA NA KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA,
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI,
(ACP) LIBERATUS SABAS
TAREHE 22/11/2012.
MAONYESHO YA SEKTA YA NYUMBA – TANZANIA HOMES EXPO KUFANYIKA MLIMANI CITY DISEMBA 7 – 9 2012.
Maonyesho
makubwa ya sekta ya nyumba ya Tanzania Homes Expo yanatarajiwa
kufanyika kwa mara ya pili Nchini Tanzania kuanzia tarehe 7 hadi 9
Disemba 2012. Kwa mara ya kwanza maonyesho ya Tanzania Homes Expo yalifanyika mwezi June na yalifungwa rasmi na Makamu wa Rais Dr Mohammed Gharib Bilal.
Akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es salaam leo, Mkurugenzi wa Tanzania Homes Expo Ndugu Zenno
Ngowi aliseme ‘’Upatikani wa makazi ya uhakika na upatikanaji wa
masuluhisho ya ujenzi wa nyumba bado umeendelea kuwa changamoto kubwa
kwa Watanzania wengi. Hata hivyo, katika kipindi hiki Nchini Tanzania
tumeshuhudia kukua kwa kasi kwa sekta ya nyumba na huduma nyingine za
ujenzi katika siku za karibuni. Hata hivyo uwepo wa taarifa sahihi juu
ya masuluhisho mbalimbali yahusuyo sekta ya nyumba limekuwa nin tatizo
kubwa, upungufu huu ndio ulikuwa msingi Mkuu wa kuanzisha maonyesho ya
Tanzania Homes Expo’’
Zenno aliongeza kusema ‘’Ni jambo
la kujipongeza kuona mabenki kadhaa yanatoa mikopo ya nyumba, lakini
taarifa za kina namna ya kupata mikopo hii raia wengi hawajui!, Je ni
mara ngapi imebidi mtu kusimamia nyumba yake mwenyewe wakati wataalam na
macontractor wapo! Je kabla ya kuchagua aina ya nyumba ya kujenga
tunajua mambo muhimu ya kuzingatia? Jibu ni hapana’’.
Tanzania Homes Expo, ni maonyesho
yenye lengo la kukuza elimu ya umma kuhusu aina mbali mbali za huduma
zinazolenga sekta hii muhimu. Lakini pia Tanzania Homes Expo inatoa
fursa kwa watoa huduma za sekta ya nyumba kama; mabenki, mikopo, bima,
wakandarasi, wachora ramani, makampuni ya nyumba, makampuni ya ulinzi,
marembo, vifaa vya ujenzi na mengi yahusuyo sekta ya nyumba kupata
nafasi ya kuelezea huduma wanazozitoa.
Tanzania Homes Expo inadhaminiwa na Azania Bank, Clouds FM, TMRC na Brand Works.
Kwa taarifa zaidi au kushiriki tembelea tovuti; www.tanzaniahomesexpo.org au tuma barua pepe info@tanzaniahomesexpo.org
TUENDELEE KUMSAIDIA ANASTAZIA
Anastazia
binti anayesumbuliwa na uvimbe wa Mguu wa kushoto ambapo amekosa fedha
za kupata angalau matibabu ya awali,napenda kuchukua nafasi hii
kuwashukuru wale wote walioonyesha kuguswa na habari hii na mpaka sasa
kuna wengine wametuma na wemetoa ahadi ya kutoa fedha za kumsaidia
Anastazia.
Mpaka sasa Mama Abduweli wa
Mamlaka ya banadari Dar es Salaama mwenye namba 0713 689656 ametuma
kiasi cha shilingi 10,000 huku dada Edna John kutoka Uingereza aliyesoma
Blog ya Michuzi amesema atatuma fedha za kumsaidia Anastazia kwenye
akaunti.
*Picha hizo zinaonyesha
Augustine Mgendi akimkabidhi Mama yake na Anastazia kiasi cha shilingi
10,000 fedha iliyotolewa na mama Abduweli wa Bandari ya Dar es
Salaam,baada ya kukabidhi fedha hizo mama huyo alishukuru na kusema kuwa
itasaidia kupiga Xray kwani hakuwa na kiasi cha shilingi 10,000 kupiga
X ray.
Hivyo basi watanzania tuendelee
kumsaidia Annastazia ili aweze kurudi katika hali yake ya kawaida
aungane na ndugu zake katika ujenzi wa familia yake,kama unamchango
wowote unaweza kupitishia katika akaunti 022201093996 NBC au katika simu
namba 0756 035 825
NIKO TAYARI KIAKILI NA KIMWILI KULITUMIKIA TAIFA: KINANA
NA BASHIR NKOROMO, RUKWA
KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman
Kinana amewahakikishia Watanzania, hususan wanachama wana-CCM kwamba
yupo tayari kimwili na kiakili kuhakikisha anatekeleza kwa ufanisi
mkubwa majukumun makubwa aliyopewa kulitumikia taifa.
Kinana alisema hayo leo kwenye
mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Rukwa akiwa katika siku yake ya
pili ya ziara ya siku nne katika mikoa ya Mtwara, Rukwa, Geita na Arusha
aliyoianza jana.
“Ni kweli nilikuwa nimetangaza
kustaafu siasa kwa kuzingatia kwamaba nimeshashika kwa muda mrefu
nyadhifa za kuchaguliwa, nikaona kwamba kama wenzako wameshakuamini mwa
muda mrefu ukafanya nao kazi wakikupenda, basi usisubiri mapaka uchokwe
ndiyo uondoke”, alisema Kinana na kuongeza;
“Lakini sasa baada ya maamuzi
yangu, Mwenyekiti wa Chama Chetu, Rais Jakaya Kikwete akaamua kwa kadiri
alivyoona inafaa, akaniteua nikisaidie Chama. Kwa mtu mwenye hekima na
uadilifu unapoteuliwa na Mwenyekiti wa Chama chako tena Rais wa Chama
kinachotawala, lazima ukubali tena bila kinyongo, nikakubali”.
“Sasa baada ya kuwa mimi ndiye
Katibu Mkuu wa Chama hiki, napenda kuwaambia kwa dhadi ya moyo wangu
kwamba nipo tayari, kimwili, kiakili kuhakikisha nawatumikia Wana-CCM na
watanzania kwa jumla kwa weledi na ufanisi mkubwa”.
Tanzania yasifiwa kwa kuongeza ufanisi katika bandari zake
Mwakilishi wa Tanzania Phares Magesa akiwasilisha mada inayohusu mfumo mpya wa eSWS katika mkutano huo
……………………………………………………………………
Katika mkutano
ulioandaliwa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshugulikia Uchumi Afrika
(UNECA) uliokuwa unafanyika Moroni, Comoro 20-21 Novemba, 2012, Mkutano
wenye lengo la kuendeleza biashara bila kutumia karatasi “Advancing
Paperless Trade in Eastern Africa”.
Tanzania ilisifiwa na wasemaji wengi wa mkutano huo kutokana na juhudi za kuimarisha miundombinu ya usafirishaji na kuongeza ufanisi katika bandari zake.Mkutano huo ulihudhuriwa na wawakilishi wa serikali na wataalamu wa masuala ya usafirishaji na Teknolojia ya habari na mawasiliano(Tehama) kutoka nchi zote za Afrika Mashariki, Kati, Kusini na visiwa vyote vya bahari ya hindi.
Mmoja wa wachangiaji mada katika mkutano huo ndugu Hamidou M’Homa ambaye ni Rais wa Chama Cha watumiaji wa huduma Comoro, alisema kwa kipindi cha karibuni ameona ufanisi umeongezeka katika bandari za Tanzania na akatoa pongezi nyingi kwa jitihada zinazofanywa na serikali na Mamlaka ya Bandari Tanzania katika kuboresha huduma.
Msemaji wa Tanzania katika mkutano huo Ndugu Phares Magesa alipokea salamu hizo za pongezi na kuelezea jitihada mbali mbali zinazofanywa na TPA na Serikali katika kuboresha huduma katika badari zetu. Moja ya jitihada hizo kwa upande wa Teknolojia ni kuanza matumizi ya mifumo ya kisasa ya kuhudumia mizigo na meli ambapo sasa watumiaji wa huduma za meli na mizigo wanaweza wakafanya kazi kutokea maofisini kwao badala wote kwena bandarini hivyo kupunguza msongamano bandarini na kurahisisha utuoaji huduma.
MIKUTANO YA UKUSANYAJI MAONI YA WANANCHI YAFANYIKA TARIME
Mjumbe
wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Humphery Polepole (aliyesimama) akitoa
ufafanuzi wa vipengele vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya
mwaka 1977 kwa wananchi wa Kata ya Mliiba, Wilaya ya Tarime mkoani Mara
wakati wa mkutano ulioitishwa na Tume hiyo leo alhamisi Nov.22, 2012.
Wajumbe wengine wa Tume, wa kwanza kulia Nassor Mohammed, Maria Kashonda
na Riziki Ngwali.
Wananchi
wa kijiji cha Mangucha Kata ya Nyanungu Wilaya ya Tarime mkoani Mara
wakifuatilia mkutano wa kukusanya maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya
uliotishwa na Tume ya Mabadlliko ya Katiba leo alhamisi Nov. 22, 2012
katika kijiji hicho.
………………………………………………………………..
Na Ismail Ngayonga
Tarime, Mara
MKAZI wa Kata ya Kata ya Mliiba
Wilaya ya Tarime mkoani Mara, Marco Magubo (31) amependekeza ni vyema
Katiba Mpya ikataze vyama vya siasa vinavyoingia madarakani mara baada
ya kushinda uchaguzi wa Rais visipeperushe bendera yake na badala yake
kuweka bendera ya Taifa.
Akitoa maoni yake leo (Alhamisi
Nov. 22, 2012) kuhusu Katiba Mpya kwa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya
Katiba alisema kitendo cha kupeperusha bendera ya chama kilichoingia
madarakani kitaongeza chuki kwa wanachama wa Chama kingine cha siasa
kilichoshindwa uchaguzi.
Aidha Magubo alisema Rais
anayeingia madarakani anawakilisha maslahi ya wananchi wote na hivyo si
busara kwa Chama kilichoshida uchaguzi kupeperusha bendera ya Chama chao
kwani Kiongozi huyo haongozi wanachama wa chama chake pekee bali
wananchi wote katika taifa.
“Tazama Marekani ambao hivi majuzi
tu walifanya uchaguzi mkuu wa Rais, katika kampeni za vyama vyao
hatukuweza kuona bendera ya Republican wala Democracy ambavyo vyote
vilishiriki uchaguzi na badala yake tuliona wananchi wakipeperusha
bendera ya Taifa lao na hatukuona bendera ya Republican wala Democracy”
alisema
Alisema kwa kuwa Tanzania ni nchi
ya umoja, amani na mshikamano ni vyema Katiba Mpya ikewe kipengele cha
kukataza bendera za vyama vyao na badala ya wamwachie Kiongozi aliyopo
madarakani kutetea hoja za wananchi wote.
FM ACADEMIA KUSHEREHEKEA MIAKA 15 TANGU KUANZISHWA KWAKE
KATIKA
kuadhimisha miaka 15 tangu kuanzishwa kwake, bendi ya muziki wa dansi
ya Fm Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ inatarajiwa kufanya onyesho la aina
yake siku ya Desemba 14 kwenye ukumbi wa Msasani Club.
Mratibu wa
onyesho hilo, Nassib Mahinya alisema kwamba, usiku huo wa aina yake
utaambatana na shamrashamra mbalimbali zilizoandaliwa ili kuwapa raha
mashabiki watakaojitokeza.
Alisema kupitia usiku huo ambao
pia utawakutanisha wasanii wote waliopata kupitia bendi tangu kuanzishwa
kwake, pia bendi hiyo itaopiga nyimbo zake kuanzia zile zilizotoka
kwenye albamu yao ya kwanza hadi sasa.
“Pia kutakuwa na tukio la kukata
keki sambamba na kuwapongeza wale wote waliochangia kwa namna moja ama
nyingine kuifikisha hapo ilipo bendi hiyo,”alisema
Mahinya aliongeza kuwa katika
kunogesha zaidi usiku huo wasanii na makundi mbalimbali wanatarajia
kusindikiza wakiwemo kundi la Mapacha watatu pamoja na wasanii wa kundi
la Mtanashati Entertauinment wakiwemo Dogo Janja, PNC na wengineo.
Onyesho hilo limeandaliwa na
Sinai Entertainment na kudhaminiwa na Mabibo Beer Wine & Spirit,
Mama Mbaga Catering, Africa Media Group, Chonapi General Supplier, Benny
Mlokozi Company , Big Solution, Mtanashati Entertainment, Eliado Point
View, Arafa Salon, Friendship Restaurant na Masters Club.
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MAADHIMISHO YA SIKU YA TAKWIMU AFRIKA, LEO DAR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mkurugenzi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Brandina Chuwa, wakati alipokuwa akiwasili kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, jana Nov 22, 2012 kwa ajili ya kufungua rasmi Maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wananchi wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika, yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, jana Nov 22, 2012. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Ofisi ya Takwimu waliokuwa Meza Kuu, baada ya kufungua rasmi Maadhimisho hayo jana. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu waliohudhuria ufunguzi wa maadhimisho hayo baada ya ufunguzi rasmi uliofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam leo. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Kamishna wa Sensa , Hajjat Amina Mrisho Said, wakati akiondoka katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, jana Nov 22, 2012 baada ya kufungua rasmi Maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika. Picha na OMR
RAIS KIKWETE AKUTANA NA RAIS MSTAAFU WA AFRIKA KUSINI MHE. THABO MBEKI
ZIARA YA RAIS WA ZANZIBA NCHINI VIETNAM
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein,akisalimiana na Maofisa wa Serikali ya Nchini Vietnam,alipowasili
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hanoi Nchini Vietnam,alipowasili
Nchni humo akiwa katika ziara rasmi ya Kiserikali.[Picha na Ramadhan
Othman Vietnam
Mke
wa Rais waZanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema
Shein,(katikati) akifuatana na Afisa Ubalozi wa Matilda
S.Masuka,(kushoto) wakati alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Hanoi Nchini Vietnam,alipofuatana na Mhe Rais wa Zanzibar
Dk.Ali Mohamed Shein,kwa Ziara Rasmi ya Kiserikali,(kulia) Msaidizi wa
Mama Shein,Ashunta Andrea.[Picha na Ramadhan Othman Vietnam.]
Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mahadhi
Maalim,(kulia) Mshauri wa Rais wa Zanzibar Ushirikiano wa Kimataifa
Balozi Ramia,na Waziri wa Kilimo Maliasili Suleiman Nyanga,wakiwa ni
miongozi mwa Ujumbe wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi nchini Vietnam,wakiwa katika Chumba cha Mapumziko cha
Viongozi VIP,katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hanoi Nchini
Vietnam,mara baada ya kuwasili nchini humo jana.[Picha na Ramadhan
Othman Vietnam.]
MAHAFALI YA TATU YA CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM) YAFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA CHIMWAGA MUDA HUU
Hii
Ndio sehemu watakayokaa wakuu na Viongozi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma
kwaajili ya kuwatunuku wahitimu muda mfupi ujao katika viwanja vya
chimwaga vilivyopo chuoni hapo
Baadhi
ya Wahitimu wa Kitivo Cha Sayansi ya Jamii, Sanaa na Lugha Cha Chuo
Kikuu Cha Dodoma wakiwa katika harakati za kutafuta picha za ukumbusho
na rafiki zao wakati wa sherehe za mahafali ya tatu ya Chuo Kikuu Cha
Dodoma yanayotajiwa kuanza saa saba Mchana wa leo katika viwanja vya
Chimwaga Vilivyopo Chuoni Hapo
Nikiwa
na Classmate wangu Wa Shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha
Dodoma Katika Mahafali ya Tatu ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM)
yanayofanyika katika Viwanja vya Chimwaga vilivyopo Chuoni Hapo
Kutoka
Kushoto Ni Josephat Lukaza Mmiliki wa Lukaza Blog akifuatiwa na
Emmanuel Mwakibinga na Patrick Kapachino Kapongwa katika Picha ya Pamoja
Kabla ya Sherehe za mahafali ya tatu ya Chuo Kikuu Cha Dodoma Kuanza
katika Viwanja Vya Chimwaga leo
Wahitimu
wakiwa katika shamrashamra za huku na kule katika Kuchuku taswira za
ukumbusho katika mahafali ya tatu ya Chuo Kikuu Cha Dodoma yanayofanyika
katika viwanja vya chimwaga vilivyopo Chuoni hapo
Wahitimu
wakiwa Katika Harakati za hapa na pale katika mahafali ya tatu ya chuo
kikuu cha Dodoma yanayofanyika katika Viwanja Vya Chiwaga Vilivyopo
Chuoni hapo leo.
Tutaendelea Kuwarushia Matukio Zaidi ya Mahafali ya Tatu Ya Chuo Kikuu Cha Dodoma. Endelea Kufuatilia Lukaza BLOG
DKT. EMMANUEL NCHIMBI KUWA MGENI RASMI UZINDUZI WA NAMBA MPYA ZA MAGARI
WAZIRI wa Mambao ya Ndani ya
Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi uzinduzi wa namba
mpya za magari ya Jeshi la Magereza. kesho asubuhi Novemba 24 mwaka
huu.
Kwa mujibu wa taarifa
iliyosambazwa kwenye vyombo vya habari na kusainiwa na Kaimu Kamishna
Jenerali wa Magereza (CP), Chamulesile, ilieleza kuwa uzinduzi huo
utafanyika kuanzia saa 4:00 asubuhi katika Gereza Kuu la Ukonga jijini
Dar es Salaam.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa
uzinduzi huo uanazingatia Sheria ya Usalama Barabarani Sura ya 162
iliyofanyiwa marekebisho ya kanuni ya Usalama Barabarani (Amendment, ya
2004.
Ilisema marekebisho hayo
yalitangazwa kwenye Gazeti la Serikali Na.102 la Machi 23 mwaka huu, na
yalitoa nguvu ya kisheria kwa magari ya Jeshi hilo kuanza kutumia namba
mpya zenye jina la jeshi hilo la Magereza.
Aidha, magari ya Jeshi la Magereza yatatambulika kirahisi wakati wa kutekeleza majukumu yake.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya udhibiti wa Manunuzi ya Umma akabidhi ripoti ya utendaji kazi
Mhe.
Waziri wa Fedha Dkt. William Mgimwa akisikiliza hotuba aliyokuwa akitoa
Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya umma
Jaji Thomas B. Mihayo
Kaimu
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya udhibiti wa Manunuzi ya Umma Jaji
Thomas B. Mihayo akikabidhi ripoti ya utendaji ya mwaka 2011/2012 kwa
Waziri wa Fedha Dkt. William Mgimwa.
Waziri
wa Fedha Dkt. William Mgimwa akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa
Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma Dkt. Ramadhani S. Mlinga kwa
uwasilishaji wa ripoti ya mwaka 2011/2012
TUME YA HAKI ZA BINADAMU YAZITAKA TAASISI KUSIMAMIA HAKI ZA BINADAMU
TUME
ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imezitaka taasisi zinazosimamia
sheria nchini kuhakikisha zinazingatia haki za binadamu na misingi ya
utawala bora ili haki iweze kupatikana kwa wakati na kwa watu wote.
Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar
es Salaam jana, na Kamishina wa Tume hiyo, Bernadeta Gambishi, wakati
alipokuwa akizindua mradi vitabu (Vitini),vya maboresho ya sheria.
Alisema kwa kuzingatia hayo
kunaweza kuharakisha upatikanaji wa haki katika makundi yote ya kijamii
nchini, kusimamia maadili na uweled wa maofisa wa sheria, pia ukuzaji
wa uhuru wa mahakama.
Gambishi alisema kimsingi mradi huo una malengo makuu sita ambayo yatatekelezwa kwa kupitia mkakati wa Kati.
Akiyataja baadhi maeneo hayo,
kuwa ni pamoja na Mfumo bora wa sheria kitaifa: lengo hilo linasimamiwa
na Tume ya kurekebisha sheria nchini kwa kushirikiana na taasisi
nyingine washirika.
Haki za Binadamu na usimamizi
wa haki hili linasimamiwa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na
upatikanaji wa haki kwa walio na uwezo mdogohilo linasimamiwa na
Taasisi zisizo za Kiserikali (NGO’S), mfano mmoja ni Chama cha Wana
Sheria Nchini (TLS).
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Sheria,
Reginald Makoko, alisema bado Watanzania wengi wanakabiliwa na uwelewa
mdogo wa sheria hali inayowafanya baadhi yao kupoteza haki zao.
Hata hivyo, tatizo hilo kwa sasa
limepungua kutokana kuwepo kwa vyama vyama vya kisheria ambavyo vinatoa
msada wa kisheria bure , malalamiko mengi kuwasilishwa huko.
MBEKI MGENI RASMI MAJADILIANO YA UONGOZI AFRIKA DAR ES SALAAM LEO
Rais
Mstaafu wa awamu ya pili ya utawala huru wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki
(kulia) akifafania jambo wakati wa Majadiliano ya duara kuzungumzia
uongozi barani Afrika na changamoto za maendeleo
uliofanyika jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Mdahalo
huo ulioandaliwa na Taasisi ya UONGOZI Tanzania, Waziri Mkuu Mstaafu,
Cleopa David Msuya. Mbeki alikuwa Mgeni Rasmi katika mdahalo huo.
uliofanyika jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Mdahalo
huo ulioandaliwa na Taasisi ya UONGOZI Tanzania, Waziri Mkuu Mstaafu,
Cleopa David Msuya. Mbeki alikuwa Mgeni Rasmi katika mdahalo huo.
Mwenyekiti wa Majadiliano ya duara kuzungumzia uongozi barani Afrika na changamoto za maendeleo,
ulioandaliwa na Taasisi ya UONGOZI Tanzania, Waziri Mkuu Mstaafu,
Cleopa David Msuya akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mdahalo huo jijini
Dar es Salaam leo.
ulioandaliwa na Taasisi ya UONGOZI Tanzania, Waziri Mkuu Mstaafu,
Cleopa David Msuya akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mdahalo huo jijini
Dar es Salaam leo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI, Prof. Joseph Semboja, akizungumza katika mdahalo huo.
Rais
Mstaafu wa awamu ya pili ya utawala huru wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki
(kulia) akikiwa mwenye tabasamu wakati Mwenyekiti wa Majadiliano ya duara kuzungumzia uongozi barani Afrika na changamoto za maendeleo ulioandaliwa na Taasisi ya UONGOZI Tanzania, Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa David Msuya akitoa ufafanuzi wa majadiliano.
Mstaafu wa awamu ya pili ya utawala huru wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki
(kulia) akikiwa mwenye tabasamu wakati Mwenyekiti wa Majadiliano ya duara kuzungumzia uongozi barani Afrika na changamoto za maendeleo ulioandaliwa na Taasisi ya UONGOZI Tanzania, Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa David Msuya akitoa ufafanuzi wa majadiliano.
waziri
Mkuu Mstaafu, Cleopa David Msuya na Mwenyekiti wa Mdahalo wa Uongozi
Afrika, pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI, Prof.
Joseph Semboja (katikati) wakimsikiliza Balozi wa kwanza wa Tanzania
nchini Afrika Kusini Ami Mpungwe ambaye kwa sasa ni mfanyabiashara na
Mwenyekiti wa Tanzanite One muda mfupi kabla ya kuwasili kwa Mgemi rasmi
wa Majadiliano ya duara kuzungumzia uongozi barani Afrika na changamoto
za maendeleo.
Mkuu Mstaafu, Cleopa David Msuya na Mwenyekiti wa Mdahalo wa Uongozi
Afrika, pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI, Prof.
Joseph Semboja (katikati) wakimsikiliza Balozi wa kwanza wa Tanzania
nchini Afrika Kusini Ami Mpungwe ambaye kwa sasa ni mfanyabiashara na
Mwenyekiti wa Tanzanite One muda mfupi kabla ya kuwasili kwa Mgemi rasmi
wa Majadiliano ya duara kuzungumzia uongozi barani Afrika na changamoto
za maendeleo.
Mawaziri
Wakuu Wastaafu wa Tanzania, Cleo David Msuya (kulia) na Salim Ahmed
Salim wakijadiliana jambo muda mfupi kabla ya kuanza Majadiliano ya duara kuzungumzia uongozi barani Afrika na changamoto za maendeleo.PICHA ZAIDI BOFYA FATHER KIDEVU BLOG.
Wakuu Wastaafu wa Tanzania, Cleo David Msuya (kulia) na Salim Ahmed
Salim wakijadiliana jambo muda mfupi kabla ya kuanza Majadiliano ya duara kuzungumzia uongozi barani Afrika na changamoto za maendeleo.PICHA ZAIDI BOFYA FATHER KIDEVU BLOG.
DKT. RAJAB RUTENGWE PAMOJA NA UKUU WA MKOA WA KATAVI NI MKULIMA WA MFANO NA WA KUIGWA
Mkuu
wa mkoa wa Katavi Mh. Dkt. Rajab Rutengwe akitoa maelezo kadhaa kwa
Mkurugenzi wa Mtandao wa Fullshangweblog Bw. John Bukuku mara baada ya
kutembelea shamba lake la miembe lililoko katika kijiji cha Mboga mkoani
Pwani.
……………………………………………
Nimesafiri na Mkuu wa Mkoa wa
Katavi Dkt. Rajab Rutengwe nikienda huko kwa mwaliko wa mkuu wa mkoa
huyo kwa ajili ya shughuli maalum ya kumuvuzisha matukio katika uzinduzi
rasmi wa mkoa huo utakaofanyika Novemba 25 mwaka huu mjini Mpanda
ukizinduliwa na Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal.
Lakini tukiwa njiani tumepitia
kwenye shamba la Mh. Dkt. Rajab Rutengwe lililoko huko Bagamoyo Mkoani
Pwani katika kijiji cha Mboga mbele kidogo ya kijiji cha Msoga nyumbani
kwa Mh. Rais Jakaya Kikwete, Mh. Dkt. Rutengwe pamoja na majukumu yake
ya uongozi katika mkoa wa katavi ni mkulima mzuri kwani shamba lake lina
ukubwa wa hekari 15 na amepanda mazao mbalimbali yakiwemo Maembe,
Mananasi, Mapapai Michungwa, mikorosho na pia anaendesha ufuganji wa
nyuki na kuku jambo ambalo limekuwa mfano kwa wakazi wa kijiji hicho.
Mh. Dkt. Rutengwe anasema kwa
kweli hawezi kununua kiwanja ambacho hakina eneo la kilimo kwani ukulima
kwake ni jambo muhimu sana na ndiyo maana aliamua kuanzisha kilimo cha
kisasa katika kijiji hicho kwa kupanda mazao mbalimbali kitu ambacho
kimemfanya kuwa mkulima wa mfano katika kijiji chetu, endelea kuangalia
matukio zaidi katika picha
Mh.
Mkuu wa mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe akizungumza na Meneja wa
shamba lake Bwana Shamba Said Hemed wakati alipotembelea samba lake
kuona maendeleo ya mazao katika shamba hilo.
Mh. Mkuu wa mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe mmoja wa mti wa miembe ambayo imeshaanza kuzaa matunda shambani humo
Kama
wageni shamabani hapo tulikaribishwa kupata tunda la Nanasi kidogo
kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi na mmiliki wa shamba hilo na kulia ni
John Bukuku Mkurugenzi Mwendeshaji wa mtandao wa Fullshangweblog.
Meneja wa Shamba na hili Bwana Shamba Said Hemed akionyesha ukubwa wa shamba hilo lenye miembe zaidi ya Elfu nne.
No comments:
Post a Comment