MAHAFALI YA KIDATO CHA NNE SEKONDARI YA MAMA CLEMENTINA WAZAZI NA WAPEWA SOMO. | |
Mwenyekiti wa shirika la mama clementina Foundation akitoa nasaha zake kwenye mahafali hayo. |
Mkuu wa Wilaya ya Bahi,Betty Mkwasa akimkabidhi mmoja wa wahitimu zawadi. |
Rodrick
Mushi,Moshi.
Kutokana
na tatizo la uhaba wa wataalamu wa fani
zinazohitaji masomo ya sayansi nchi jitihada mbali mbali imeelezwa kuwa zinahitaji
kuanzia kwa wazazi kushirikiana na waalimu katika kuwashauri wanafunzi kuchagua
michepuo ya kusoma ili kusaidia
kuondokana na tatizo hilo.
Akizungumza
kwenye mahafali ya kidato cha nne ya shule ya sekondari Mama Clementina
Foundation mwenyekiti wa shirika la Mama Clementine Foundatin Maria Josephine alisema nchi ina tatizo la
wataama kama Madaktari,mafamasia,wataalamu wa kilimo,wahasibu,maafisa biashara
pamoja na fani nyingin zinazohitaji elimu ya sayansi.
Alisema
kuwa wanafunzi wengi wamekuwa wakisoma masomo ambayo inakwua rahisi kwao kuweza
kufaulu huku akitolea mfano michepuo kama ya Mahusiano ya Umma,Maendeleo ya
Jamii utawala na michepuo mingine huku uhaba ambao umekuwa wa wataalamu
ukiendelea kuongezeka.
Maria
Alisema kuwa kutokana na tatizo hilo kuwa kubwa mikakati mbalimbali inahitajika
ikiwa ni pamoja na kuinua na kuyapa kipaumbelea masomo ya sayansi na
biashara,na wazazi kuwa karibu kuwaeleza faida za kuchukua michepuo hiyo ambayo
pia imekuwa na nafasi kubwa ya ajira.
“Tatizo
linalokabili nchi yetu ni tatizo la uhaba wa wataalamu,na wataalamu wanaohitaji
ni muhimu na ili nchi iendelee lazima Nyanja hizo wawepo wataalamu wa kutosha
hivyo suala hilo Serikali na wadau wengine kama wazazi na waalimu wanapaswa
kushiriana kulimaliza”Alisema
Katika
hatua nyingine alisema tatizo hilo linanzia mashuleni kwa wanafunzi kushindwa kufanya
vizuri katika masomo ya sanyansi kama phisikia,kemia baologia na hesabu huku
idadi ya wanaoshidnwa kufanya vizuri wakiwa ni wasichana,ambapo wanafuzni ambao
wamekuwa wakifanya vizuri ni wale wanaosoma shule binafsi.
Kwa
upande wake Mgeni rasmi kwenye mahafali hayo Mkuu wa Wilaya ya
Bahi Betty Mkwasa alitoa wito kwa
wamiliki wa shule binafsi kuwa na tabia ya kujitolea kuwasomesha baadhi ya watoto
ambao wazazi hawana uwezo au yatima kama ambavyo shule hiyo ya mama Clementina
imekuwa ikifanya.
“Kuna wamiliki wa shule binafsi ambao
wamewasahau kabisa watoto maskini lakini ukweli ni kwamba ukimsaidia maskini
utapa Baraka kwa Mungu lakini pia umesaidia kujenga taifa kwani motto mmoja
unayemsaidia anaweza kuja kuikomboa jamii yake”Alisema Mkwasa.
Mwisho
No comments:
Post a Comment