HIVI NDIVYO ZITO KABWE ALIVYOFUNGA KAMPENI ZA UCHAGUZI KILIMANJARO.
Asema kiama cha Vigogo walioficha mabilioni Uswisi kinakuja.
Tayari kuwasilisha hoja binafsi mabilion hayo yarejeshwe.
|
Mgombea Udiwani wa Kata ya Nanjara reha,Frank Salakana akiwa amebebwa na wapiga kura wake wakati wa kufungwa kwa kampeni ambapo uchaguzi unafanyika leo. |
|
Zito Kabwe akitema cheche zake,ambaye ndiye aliyekuja kwa ajili ya kufunga kampeni hizo. |
|
Zito akimnadi Mgombea Udiwani,Frank Salakana. |
|
Zito akimnadi mgomnbea ubunge wa Kata ya Kilema Kusini,Severine wakati wa kufungwa kwa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani. |
|
|
Zitto: Vigogo walioficha mabilioni Uswisi kukiona
• Aandaa hoja binafsi bungeni kutaka zirejeshwe
na Rodrick Mushi, Rombo
WAKATI serikali ikishindwa kuwataja vigogo walioficha mabilioni ya
fedha nchini Uswisi, Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Kabwe,
anatarajia kuwasilisha hoja binafsi katika mkutano wa tisa unaotarajiwa
kuanza wiki ijayo mjini Dodoma, kutaka serikali irejeshe fedha hizo.
Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, amesema tayari hoja hiyo imeshapata baraka za Spika wa Bunge, Anne Makinda.
Mbunge huyo wa CHADEMA alisema hayo jana wakati wa akifunga mkutano wa
kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani wa Kata ya Nanjarareha, wilayani
Rombo, mkoani Kilimanjaro.
Katika uchaguzi huo unaotarajiwa
kufanyika leo, CHADEMA imemsimamisha, Frank Salakana. Alisema sh bilioni
349 zilizofichwa Uswisi na baadhi ya vigogo wa serikali ya Chama cha
Mapinduzi (CCM), lazima zirejeshwe nchini, huku akimtaka Mkurugenzi wa
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Edward Hosea,
kueleza umma barua aliyoituma nchini humo kwa ajili ya kashfa hiyo
ilikuwa na lengo gani.
Alisema barua ya Dk. Hosea imesababisha
ugumu wa upatikanaji wa taarifa za mabenki ya nchini Uswisi ambayo
yameshindwa kutoa ushirikiano kwa kamati inayofuatilia kashfa hiyo.
Huku akishangiliwa na maelfu ya wanachama wa CHADEMA waliofurika
kusikiliza mkutano huo, Zitto alisema wizi wa mabilioni hayo umetokana
na kuporomoka kwa maadili ya viongozi nchini ambao wengi wanajali zaidi
masilahi binafsi badala ya umma.
Mbunge huyo machachari wa
CHADEMA, alisema kuna haja kama taifa kurejesha maadili ya uongozi kama
enzi za utawala wa Mwalimu Nyerere ili viongozi wachague kitu kimoja,
kati ya biashara na siasa.
Alisema CHADEMA imepania kuhakikisha
mabilioni hayo yanarejeshwa ili yaweze kutumika kuwasaidia Watanzania
katika kujenga na kuboresha miundombinu ya barabara, maji na afya.
Aliwataka viongozi walioficha mabilioni hayo kujitokeza mapema na kueleza jinsi walivyozipata badala ya kusubiri kuumbuliwa.
“Nawataka viongozi waliohusika wajitokeze wenyewe, waeleze
walivyozipata na kisha wazirejeshe nchini, vinginevyo patachimbika,
kwani nitahakikisha kama chama tunashirikiana na Benki ya Dunia
kuhakikisha fedha hizo zinarudi nchini,” alisema Zitto.
Alisema
CHADEMA inapigania fedha hizo zirejeshwe kwani zimetokana na wizi wa
rasilimali za Watanzania kupitia mikataba mibovu ya mafuta na wizi wa
madini na nyingine.
Katika ripoti ya Swiss Central Bank,
iliyotolewa hivi karibuni, inaonesha kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi
11 barani Afrika ambazo vigogo wake wa kibiashara, kitawala na kisiasa
wameficha kwa siri mabilioni ya fedha katika mabenki ya Uswisi.
Nchini nyingine za Afrika zilizoficha fedha hizo ni Kenya, Uganda,
Zimbabwe, Misri, Shelisheli, Afrika Kusini, Rwanda, Sierra Leone,
Somalia na Sudan.
Kwa upande wa Tanzania, mapesa ambayo yamefichwa huko ni dola milioni 196.87, sawa na shilingi za Tanzania bilioni 315.5!
Hebu jiulize; mapesa haya tuliyoibiwa yangetusaidia kiasi gani kama
yangerejeshwa nchini na kutumbukizwa kwenye miradi ya kuboresha huduma
za jamii?
Pia jiulize swali jingine: Je, hata baada ya Benki
Kuu ya Uswisi kuturahisishia mambo kwa kututobolea ukweli kwamba
tumeibiwa, na kwamba wezi wetu wameficha hizo fedha nchini mwao,
watawala wetu wana dhamira ya kuanzisha mchakato ili wahusika wafikishwe
mahakamani na fedha hizo zirejeshwe nchini?
No comments:
Post a Comment