Uchumi wa eneo la West Kilimanjaro Wilatani Siha umekuwa kutokana na mazao yanayolimwa karibia mwaka mzima yakiwemo viazi na Caroti ambazo wakulima hujipatia vipato |
Meneja wa Msitu wa West Kilimanjaro Bakari Mohamedi wakati akizungumza na blog ya
Tanzania Leo.inayoonekana ni miche ya miti.
Kuwepo kwa ushirikiano mzuri baina ya uongozi wa msitu wa West Kilimanjaro na wananchi wanaouzunguka msitu huo umesaidia kuendelea kuboresha msitu huo pamoja na wananchi kujipatia kipato.
Blog hii ya tanzania leo akiongea na meneja wa msitu huo Bakari Mohamedi alisema kuwa wamejiwekea mazingira mazuri na mahusiano kwa wananchi kwa lengo la kuwatumia wananchi kuulinda msitu kama mali yao.
Alisema Wananchi 15,000 kutoka Wilaya mbalimbali za Mkoa wa
Kilimanjaro wananufaika na kilimo cha mazao mmbalimbali kwa nyakati tofauti
katika msitu wa West Kilimanjaro Uliopo Wilayani Siha.
Alisema kuwa wananchi kutoka katika Wilaya za
Rombo,Hai,Siha,na maeneo mengine hupata fursa ya kulima mazao kama
viazi,mbogamboga,karoti mahindi maharage baada ya misitu kuvunwa.
Pia wakulima zaidi ya 7000 huweza kuingia kila siku
kwenye msitu wa huo na kuweza kujipatia riziki kwa kufanya kazi mbalimbali
ndani ya msitu,ikiweno wanaonunua,wanaosafirisha mazao yanayolimwa ndani ya
Msitu.
Bakari alisema kuwa wakulima wanaogaiwa sehemu kwa
ajili ya kilimo huweza kulima kwa muda wa miaka 5 na hivyo kuweza kujipatia
kipato.
Alisema kuwa ugawaji wa maeneo kwa wananchi kwa ajili
ya kilmo huzingatia pia makundi maalumu katika jamii hususani wasiojiweza na
wanaoishi na virusi vua UKIMWI ili kuweza kujipatia riziki.
Aliongeza kuwa ushirikiano huo mzuri umekuwa ukisaidia
kwa uongozi wa msitu kupata taarifa kwa baadhi ya wananchi ambao wamekuwa
wakijaribu kuharibu mazingira pamoja na kuvamia msitu.
“Wananchi ambao tumekuwa tukiwapatia maeneo kwa
ajili ya kilimo wamekuwa wakitusaidia kupambana na watu ambao wanaharibu msitu
pamoja na kuzuia upikaji wa gongo ndani yam situ”Alisema Bakari.
Mbali na hayo pia alisema ushirikishwaji huo wa
wananchi umekuwa ukipunguza idara yam situ garama za usafishaji wa msitu baada
ya uvunaji pamoja na upaliliaji wa wa miti baada ya kupandwa.
|
No comments:
Post a Comment