WAZIRI MAIGE AKIWA KWENYE MOJA YA ZIRA ZAKE MKOANI IRINGA HAPA ANAZUNGUMZA NA WANANCHI WA MATAMBA MAKETE KWENYE MKUTANO WA HADHARA.
Waziri wa maliasili na utalii Ezekiel Maige asema kuwa msitu wa Sao Hill
Mufindi umechangia kwa kiasi kikubwa kushusha umaarufu wake wa
utendaji kutokana na siasa iliyoingizwa katika msitu huo .
Pia alisema kuwa kamwe hatafanya kazi kwa kukurupuka bali atazingatia maoni ya wananchi na taratibu za nchi huku akidai kuwa hategemei Kama wavunaji wakubwa katika msitu wa Sao Hill Mufindi watakuwa na wavunaji milele . Huku akisisitiza Kuwa asilimia 80 ya maamuzi ya wizara yatatokana na mawazo mazuri ya wavunaji hao wadogo wadogo. Waziri Maige ametoa kauli hiyo leo katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Mufindi ,wakati wa kikao chake na wavunaji wadogo wadogo katika msitu huo wa Sao Hill. Pia asema wazo na mashine ndogo kwa upande wake anashawishika kuliacha Kama lilivyo ila ofisi yake haita kuwa na huruma kwa wale wasio na mashine. Asema kuwa mashine vinapaswa kuwa na Kikomo katika msitu huo japo kuna haja ya mtendaji mkuu wa TFS kufika na kukutana na wavunaji hao ikiwa ni pamoja na kuunda Kamati ya ushauri itakayowezesha kupokea maoni ya wahusika. Asisitiza kuwa lazima wavunaji wakubwa kupewa vibali kulingana na mahitaji hivyo lazima watakuwa na Kikomo cha kupewa miti tofauti na ilivyo sasa. Asema kuwa wavunaji wakubwa lazima wapande miti ili kuondoa tatizo la miti na kuwa kuna haja ya wavunaji hao wakubwa kuwa na mashamba yao badala ya kutegemea kuvuna miti iliyopangwa. Alisema asilimia 68 ya mbao zote nchini inatokana na misitu ya Serikali hivyo katika hali hiyo lazima kuwepo kwa kasi ya upandaji na kuwa kutokana na mikakati inayoendelea kufanywa sasa lazima mbele ya safari asilimia 40 ya mbao itokane na misitu ya watu binafsi. Waziri Maige alisema kuwa kuna haja ya serikali kuzungumza na Chama cha wavunaji wadogo wadogo katika msitu wa Sao Hill (SAFIA) kupewa ardhi kwa ajili ya Kupanda miti ila hati ya umiliki kuwa chini ya serikali . habari na Francis Godwin Iringa |
Sunday, March 18, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment