WIZARA YA MALI ASILI NA UTALII KUSAIDIA SHINDANO LA MISS UTALII
Waziri wa Mali Asili na Utalii Ezeckiel Maige.
WIZARA INAYATHAMINI MASHINDANO YA MISS UTALII
Wizara
ya Maliasili na Utalii inaunga mkono Mashindano ya Miss Utalii na kuwa
iko tayari kushirikiana na taasisi yoyote ya Sekta Binafsi ambayo
itakuja na mikakati mizuri ambayo italenga katika kufanikisha maandalizi ya dhati ya kufanikisha mashindano hayo.
Msimamo
huu umetolewa na Wizara kufuatia makala iliyochapishwa na gazeti la
Mtanzania toleo la tarehe 7/4/2012 katika safu ya Wazo Binafsi yenye
kichwa cha habari: ‘Serikali isichezee Shindano la Miss Utalii
Tanzania’.
Wizara
inasisitiza kuwa inathamini mashindano ya Miss Utalii na kamwe
haitayachezea. Tangu shindano hilo lianze Wizara imekuwa ikiliunga mkono
kupitia Bodi ya Utalii Tanzania (TTB). Pia Waziri wa Maliasili na
Utalii amekuwa Mgeni Rasmi mara kwa mara katika hafla mbalimbali za
mashindano hayo.
Wizara imekuwa ikihimiza Sekta
Binafsi kutekeleza Sera ya Taifa ya Utalii kwa kubuni na kufanya
shughuli mbalimbali zenye manufaa kwao na kwa taifa kwa ujumla, kama
vile kuwekeza kwenye biashara ya hoteli , usafirishaji watalii na
kutangaza utalii kwa njia mbalimbali.
Mashindano
ya Miss Utalii ni njia moja wapo nzuri ya kutangaza utalii ndiyo maana
Wizara inayaunga mkono. Ndiyo maana Wizara inaitaka Sekta Binafsi
kuandaa mkakati mpya utakaolenga katika kufanikisha mashindano hayo na
Wizara itatoa ushirikiano unaofaa.
George Matiko
MSEMAJI
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
No comments:
Post a Comment