
Rais Jakaya Kikwete akitangaza majina ya wajumbe wa Tume ya katika
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete atazindua rasmi Tume ya Kukusanya na Kuratibu Maoni ya
Mabadiliko ya Katiba na kuapisha wajumbe wa Tume hiyo Ijumaa ijayo,
Aprili 13, mwaka huu, 2012.
Tume hiyo itazinduliwa na wajumbe wake kuapishwa kulingana na matakwa
ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011 iliyounda Tume hiyo.
Aidha, Tume hiyo itazinduliwa rasmi wiki moja baada ya kuwa imetangazwa
rasmi. Rais Kikwete alitangaza Tume hiyo jana, Ijumaa, Aprili 6, 2012,
kwenye mkutano wa wahariri uliofanyika Ikulu, Dar es Salaam.
Tume hiyo itakayoongozwa na Mwenyekiti Jaji Joseph Sinde Warioba
akisaidiwa na Makamu Mwenyekiti Jaji Mkuu Mstaafu, Jaji Augustino
Ramadhan ina wajumbe 30, ikiwa ni wajumbe 15 kutoka kila moja ya pande
mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wajumbe wa Tume hiyo kutoka Tanzania Bara ni Profesa Mwesiga L
Baregu, Ndugu Riziki Shahari Mngwali, Dkt. Edmund Adrian Sengodo Mvungi,
Ndugu Richard Shadrack Lyimo, Ndugu John J Nkolo, Alhaji Saidi El
Maamry na Ndugu Jesca Sydney Mkuchu.
Wajumbe wengine wa Tume hiyo kutoka Bara ni Profesa Palamagamba
Kabudi, Ndugu Humphrey Polepole, Ndugu Yahya Msulwa, Ndugu Esther
Mkwizu, Ndugu Maria Malingumu Kashonda, Mheshimiwa Al-Shaymaa J Kwegyir,
Ndugu Mwantumu Jasmine Malale na Ndugu Joseph Butiku.
Wajumbe wa Tume hiyo kutoka Tanzania Visiwani ni Dkt. Salim Ahmed
Salim, Ndugu Fatma Saidi Ali, Ndugu Omar Sheha Mussa, Ndugu Raya
Suleiman Hamad, Ndugu Awadh Ali Saidi, Ndugu Ussi Khamis Haji na Ndugu
Salma Maoulidi.
Wengine kutoka Visiwani ni Ndugu Nassor Khamis Mohammed, Ndugu Simai
Mohammed Said, Ndugu Muhammed Yussuf Mshamba, Ndugu Kibibi Mwinyi
Hassan, Ndugu Suleiman Omar Ali, Ndugu Salama Kombo Ahmed, Ndugu
Abubakar Mohammed Ali na Ndugu Ally Abdullah Ally Saleh.
Shughuli za Tume hiyo zitaratibiwa na Sekretarieti ambayo Katibu wake
atakuwa Ndugu Assaa Ahmad Rashid na Naibu Katibu atakuwa Ndugu Casmir
Sumba Kyuki.
Mwisho.
Imetolewa na:Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,Ikulu.
No comments:
Post a Comment