Misaada yawasili Indonesia
Mkaazi wa kisiwa cha Mentawai magahribi mwa Sumatra
Misaada imeendelea kuwafikia
wale waliokumbwa na maafa Indonesia baada ya meli tatu kufika katika
kisiwa kilichoharibiwa zaidi na tsunami.
Vikosi vya uokoaji sasa wanajitahidi kusaidia watu katika kisiwa cha Pagai Kaskazini magharibi mwa Sumatra.
Inafahamika kuwa zaidi ya watu 340 wamefariki dunia.Mamia bado hawajulikani walipo.
![]() |
Rais Susilo Bambang Yudhoyono atembelea visiwa vilivyoadhiriwa na tetemekolikatiza safari
yake huko Vietnam ili kusimamia shughuli ya uokoaji,na alisafiri kwa
helikopta ambayo ilikuwa imebeba vyakula na bidhaa zengine muhimu.
Huko alikutana na wale walionusurika pamoja na viongozi wa eneo hilo.
Ameahidi kuwa serikali itasaidia utawala wa
Sumatra Magharibi kujenga nyumba za muda, vituo vya afya na shule,
msemaji wake alisema.
Msaada huo umefika huku Indonesia ikikabiliana na maafa mengine yaliyoletwa na mlipuko wa mlima Merapi katikati mwa Java.Zaidi ya 30 waliuawa.
No comments:
Post a Comment