MANGI WA MARANGU FREANK MAREALLE ALIYEVALIA KOFIA YA ASILI,AKIPENA MKONO NA KAKA YAKE AMBAYE NI MWENYEKITI WA UKOO WA MAREALLE WILFRED MAREALLE BAADA KUMALIZIKA KWA KUSIKILIZWA KWA ZUIO LILOKUWEPO MAHKAMANI HAPO.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Manispa ya Moshi
imetupilia mbali zuio lililokuwa limefunguliwa mahakamani hapo,la kuzuiwa
kusimikwa kwa mangi wa Marangu Frank Marealle,pamoja na zuio la kula chakula
cha mchana na wana marangu.
Zuio hilo lilikuwa limefunguliwa mahakamani hapo na
Anita Augustine Marealle,na Willuum Marealle,wakizuiwa kuapishwa kwa Frank
Marealle kuwa Mangi wa Marangu.
Akisoma maamuzi hayo mahakamani hapo Munga Sabuni ambaye ni
hakimu mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi amesema kuwa hakuna,kesi ya kujibu
kututokana na walaliamikaji kuwasilisha maombi ya zuio bila kufungua kesi.
Sabuni amesema kuwa hadi mahakama kufikia uamuzi wa
kutupilia mbali maombi hayo ni kutokana na sheria kutaka kuwepo kwa kesi ya
msingi ambayo ingekuwa imefunguliwa na Willium Mareale na Anita Marealle mbali
na ombi la zuio.
Kwa upande wa wakili wa upande wa utetezi Albert
Msando amesema kuwa,endapo zuio hilo lisingeweza
kuendelea kupewa nguvu kutokana na walalamikaji kutofuata sheria, huku akisema
kuwa mahakama isingeweza kuendelea
kusikiliza maombi madogo mahakamani kama hakuna kesi ambayo tayari ilikuwa imefikishwa
mahakaman.
|
No comments:
Post a Comment