MKURUGENZI WA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA MAJI TAKA MUWSA ANTHONY KASONTA(KATIKATI)AKIFURAHIA ZOEZI HILO LA UPANDAJI MITI.
Imeelezwa kuwa endapo uharibifu wa mazingira
ukiendelea kufanyika Mkoani Kilimanjaro kuna hatari ya ukame wa kuendelea
kuongezeka,tofauti na hali ilivyo sasa ambayo imechangia kukauka kwa vyanzo vya
maji na mabadiliko hewa yanayosababisha kuwepo kwa joto kali.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Mamlaka
ya Maji safi
maji na maji taka Mjini Moshi(MUWSA)Anthony Kasonta wakati wa zoezi la upandaji
miti kwenye chanzo cha maji cha shiri kilichopo Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro.
Amesema kuwa hali ya upatikanaji wa maji siyo nzuri licha
ya kuwepo kwa mvua zilizonyesha hivi karibuni kutokana na ukame ambaoo ulikuwa umesababishwa na uharibifu wa
mazingira kwa kukata miti ovyo ambayo imesababisha kukaukwa kwa uoto wa asili
na vyanzo vya maji.
Alisema kuwa zoezi hilo la kupanda miti kwenye vyanzo vya maji
litakua endelevu,pamoja na kumuunga mkoni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas
Gama katika jitihada za kutunza mazingira kwa kupiga vita ukataji wa miti na
kupanda miti.
Akizungumzia suala la uhaba wa maji lililosababishwa
na ukame hivyo kuwepo kwa mgao wa maji kwa manispaa ya Moshi,hali ya
upatikanaji wa maji bado haijarudi katika hali ya kawaida licha ya mvua
zilizonyesha siku za hivi karibuni hivyo kusema bado mgao huo unaendlelea ila
hauna makali kama ilivyokuwa awali.
Jumla ya miti 600 ilipandwa katika chanzo
hicho cha maji ambayo itatunzwa na mamlaka hiyo,huku akisema kuwa mwanzo wa
maji katika vyanzo vilivyopo mbali kama mlima
Kilimanjaro hivyo wananchi wanatakiwa kutunza
mazingira bila kujali kwamba kuna chanzo cha maji au hamna.
Kasonta alisema kuwa suala la uharibifu wa
mazingira ndilo lilipolekea kuwepo kwa mgao wa maji ambao ni mara ya kwaza mgao
wa maji kuwepo Mjini hapa,huku akisema mazingira yasipotunzwa kizazi kinachokuja
kinaweza kukosa kabisa maji pamoja na miti.
|
No comments:
Post a Comment