Saturday, June 9, 2012

 YA DUNIA NI MENGI ,MTOTO SOFIA APATIKANA BAADA YA KUWEKWA MSUKULE WILAYANI TANDAHIMBA

BI MARIAM MOHAMED MAMA WA SOFIA AKIWA NA MWANAWE PAMOJA NA
BI RUKIA AKILI SALUM, MGANGA ALIEFANIKIWA KUMTOA MTOTO HUYO
ALIEFADHIWA SHIMONI KWA TAKRIBANI SIKU 18
SOFIA HAMISI AKIWA KATIKA PICHA NA MGANGA WAKE MARA BAADA YA
AKILI YAKE KURUDI KATIKA HALI YA KAWAIDA
.SOFIA HAMIS AKIWA MWENYE FURAHA BAADA YA KUPATA
TIBA KWA MGANGA WA KIENYEJI, BI RUKIA AKILI SALUM BAADA YA MGANGA HUO
KUFANIKIWA KUMTOA MTOTO HUYO ALIWEKWA MSUKULE KATIKA KIJIJI CHA MMEDA TANDAHIMBA


Mtoto Sofia Hamis mwenye umri wa miaka 12 anayesoma darasa la pili
katika shule ya Msingi Litehu wilayani Tandahimba,Mkoani Mtwara
ambaye alitoweka mwanzoni mwa MWEZI huu amepatika akiwa katika shimo
lililo katika msitu wa kijiji cha Mmeda wilayani humo huku akiwa hai
baada ya jitihada zilizofanywa na Mganga wa kienyeji kutoka kijiji cha
Mtama Lindi Vijijini

Mtoto huyo alitoweka nyumbani kwa Mama yakeMzazi tarehe 08/05/2012
akitokea shuleni na toka siku hiyo hakukuwa na taarifa za kuonekana
kwake na jitihada mbalimbali za kumpata mtoto huyo kutozaa matunda
huku siku zikisonga mbele
 Kufuatia kupotea kwa mtoto huyo kulizaa taharuki mbalimbali kijijini
hapo hali iliyomfanya mama mzazi kuhangaika kutafuta kwa njia ya imani
za jadi na kufanikiwa kujuzwa na mganga alietambulika kwa jina la
Rukia Akili Salum mkazi wa Mihogoni-Mtama Lindi Vijijii kuwa mtoto
yupo hai na anao uwezo wa kumtoa katika mazingira aliyokuwepo

Mama wa Mtoto huyo alifanikiwa kusafirisha mganga huyo hadi kijiji cha
MMEDA -kilichopo kata ya LITEHU Tandahimba ambapo baada ya kufanya
shughuli zake alifanikiwa kwa pamoja kumkuta mtoto huyo akiwa shimoni
akiwa hawezi kuongea vizuri huku mwili ukitawaliwa na upele


Baada ya kufanikiwa kumpata mganga huyo alisafiri nae kwenda Mtama
kwenye makazi yake ili ampatie tiba ambazo hadi Mimi namfikia mtoto
huyo alikuwa tayari amerudi katika hali yake ya kawaida
 Na Francis Godwin
 

No comments:

Post a Comment