Monday, June 18, 2012

AJALI YAUA WATANO NA KUJERUHI 14 KILIAMANJARO..
 
Watu watano  wamefariki dunia huku wengine 14 wakijeruhiwa vibaya baada ya gari walilokuwa wakisafira kuacha njia na na kupinduka.

Akitoa taarifa ya ajali hiyo Kaimu Kamanda wa polisi Mkoani Kiliamanjaro Ramadhani Ng’anzi alisema kuwa ajali hiyo ilitokea majira ya saa 7:00 asubuhi katika eneo la Mbosho barabara ya kware Nguni Kata ya Masama Wilayani Hai.

Alisema kuwa  ajali hiyo ilitokea jana june 17 baada ya gari lenye namba T 179 AAX Toyota Hiace  kuacha  njia gafla na kupunduka,huku dereva aliyekuwa akiendesha akitorokea kusikojulikana.

Nga’nzi Alisema kuwa gari hilo lilikuwa likitokea kware kuelekea boma na watu wote waliokuwa wamepanda kwenye gari hilo walikuwa ni abiria,waliokuwa wanaelekea boma,ambapo watu watatu walipoteza uhai eneo la ajali.

Kamanda Ng’anzi aliwataja  waliopteza maisha kwenye ajali hiyo kuwa ni Eliliwanga lema(90)mkazi wa isuki,Fred Tarimo(23) Mkazi wa masama,Rafael kimaro(66)mkazi wa losaa,Richard Munuo(55)mkazi wa nguni,pamoja na Baraka Nko(45) Mkazi wa Arusha.

Waliojeruhiwa kwenye ajali hiyo Oscar Siao (45),Alesinda Traeli (50) Leinard munis (32),Husen abdi (63),Amin adabu  Munuo (49) Richard Arnold (18)Devid Joshua (36), Mary witness (44),Walter Rabiel(37),Noel onesmo (9), Elena ngunda (60) Oisael anankya (70)  wilinad amos(37)wengi wao wakiwa ni wakazi wa Hai.

Kamanda alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi,uliodababisha gari hilo kupoteza mwelekeo na kupinduka.

Hata hivyo alisema kuwa uchunguzi wa ajali hiyo unaendelea,huku miili ya marehemu ikiwa imehifadhiwa hospitali ya kibongoto na majeruhi wakiendelea kupata matibabu hospitali ya rufaa ya KCMC.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment