Tuesday, May 29, 2012

       
CUF YAWATAKA WAFUASI WAKE NA WANANCHI ZANZIBAR KUWA WATULIVU, WAVUMILIVU NA KUTOA MAWAZO YAO BILA JAZBA

Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar na katibu Mkuu wa chama cha CUF Maalim Seif Sharif Hamad.
 
Na Juma Mohammed,MAELEZO Zanzibar
Chama cha Wananchi(CUF) kimewataka wananchi kutulia na Serikali kufanya uchunguzi wa kina kubaini chanzo cha vurugu zilizotokea mwishoni mwa wiki Mjini Zanzibar.
Taraifa ya Chama hicho kwa vyombo vya habari iliyotiwa saini na Mkurugenzi wa Uenezi na Mahusiano na Umma,Salim Bimani ilisema “Chama cha CUF kinatoa wito kwa wananchi wote kuwa watulivu, wavumilivu na kuitumia fursa ya kutoa mawazo yao bila jazba na kutowanyima wengine nafasi ya kuwasilisha mawazo yao”
Taarifa hiyo ilisema kwamba vitendo vya watu wachache kuchoma makanisa moto na kuharibu mali za watu ni vya uvunjifu wa sheria na kinyume na utamaduni wa Kizanzibari.
“Uchunguzi wa kina ufanyike na waliohusika wachukuliwe hatua za kisheria bila uonevu wala upendeleo” Alisema Bimani katika taarifa yake hiyo ambayo pia alisema kwamba ni lazima kwa wakati huu na kwa haraka iwezekanavyo, Serikali izungumze na Mashekhe bila ya kuona muhali na kwa uwazi kabisa ili kutafuta suluhu ya kudumu kwa faida ya nchi.
Chama hicho kimesema kwamba pamoja na sababu au visingizio mbalimbali vilivyotajwa kuwa chanzo cha hali hiyo, zikiwemo za hamasa za wananchi, chuki binafsi, ukosefu wa hekima,matumizi ya nguvu za dola na hata uchochezi wa makusudi wa wale wanaoonekana kutokupendelea maridhiano ya kisiasa Zanzibar.
“Chama cha Wananchi,CUF, kama sehemu muhimu ya Umma wa Watanzania,hakiwezi kukaa kimya kutokana na mwelekeo mzima wa hali tete ya amani katika nchi, ingawa ni dhahiri wapo baadhi ya watu wasioitakia mema Zanzibar wakibainika kufurahia mazingira hayo,kwa maslahi binafsi na pia kutoa kauli za kutatanisha za kisiasa” Alisema Bimani katika taarifa yake.
 

TANZANIA YAUNGANA NA NCHI NYINGINEZO DUNIANI KUADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA WALINDA AMANI WA UMOJA WA MATAIFA

 
 
Mgeni rasmi Naibu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Mahadhi Juma Maalim na Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) hapa nchini Bibi. Hopolang Phororo na UwaGeneral Officer Commanding (GOC) Meja Jenerali Hassan Vuai Chema akitoa heshima zake.  wakishiriki kuimba wimbo wa taifa katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya walinda amani  Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa inayoadhimishwa kila Mwaka tarehe 29 Mei. Picha zote na MO BLOG
Mgeni rasmi Naibu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Mahadhi Juma Maalim  akiweka shada la maua katika mnara wa kumbukumbu ya mashujaa.
Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) hapa nchini Bibi. Hopolang Phororo akiweka Shada la Maua kama ishara ya kuwakumbuka walinda Amani wa Afrika.
 
MKUTANO WA KITENGO CHA URITHI WA BAHARINI ZANZIBAR
Mkuu wa Makumbusho ya Mnazi mmoja Zanzibar Ameir Ibarahim Mshenga akionesha picha ya Watafiti wa mambo ya bahari waliyofanya Zanzibar katika kikao cha k kujadili suala la uharibifu wa mambo ya bahari kilichofanyika leo ukumbi wa Makumbusho ya Kasri uliopo Forodhani
 (Picha na Iddy Haji-Maelezo Zanzíbar)
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar  
Kamishna wa Utamaduni na Michezo Zanzibar Hamadi Bakari Mshindo amesema ipo haja ya Kitengo cha Urithi wa Baharini kuwa makini na jasiri katika kusimamia vyema urithi wa Zanzibar kwani kitengo hicho kinaweza kuwa sehemu muhimu ya kuvutia watalii ambao wanaweza kuzuru maeneo ya urithi huo.
Amesema maeneo ya Urithi wa Bahari ni sehemu muhimu kwani Wageni kutoka nchi mbalimbali wamekuwa wakiyatembelea ili kujua historia ya maeneo hayo jambo ambalo linaweza kuwa kichochoe kikubwa cha kuongeza wageni ambao huja kuitembelea Zanzibar kila msimu.
Kamishna Mshindo ameyasema hayo katika kikao cha kujadili suala la uharibifu wa mambo ya bahari kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Makumbusho ya Kasri uliopo Forodhani mjini Zanzíbar.
Amesema lengo la kikao hicho ni kujadili njia nzuri za kuhifadhi urithi wa baharini ambao kama utawekewa mikakati mizuri unaweza kuisaidia Zanzíbar kupiga hatua kwani ni eneo muhimu la kuvutia watalii.
Kamishana amesema kutokana na umuhimu wake kuna haja pia ya wadau walioshiriki katika kikao hicho kuwa na mkakati wa pamoja wa kuhakikisha mazingira ya urithi huo yanahifadhiwa kwa ajili ya maslahi ya taifa.
Amefahamisha kuwa Urithi huo ni pamoja na Meli ambazo zilizama katika bahari, mapango na vitu ambavyo vimekuwa vikitupwa katika bahari mambo ambayo yanageuka kuwa urithi ambapo watu kutoka maeneo mbalimbali huwa na hamu ya kujua historia ya vitu hivyo.
Aidha urithi huo huchangia kuongezeka kwa mazalio ya viumbe hai wa bahari ambao hugeuza maeneo hayo kuwa nyumba zao za kujihifadhia na hivyo kusababisha ongezeko la samaki.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Kale Dkt.Amina Ameir amesema kuna haja ya jamii kuelimishwa juu ya umuhimu huo sambamba na kuacha tabia ya kuchukua mabaki ya urithi huo kwa lengo la kwenda kuuza mabaki hayo kwa watu wasio husika.
Amesema kuna Wazamiaji ambao hutumiwa na watu kwa lengo la kuzamua mabaki ya Meli na Mamboti ambayo yalizama na kwenda kuyafanya bishara ya chuma chakavu jambo ambalo ni kinyume na taratibu za kisheria.
Ameongeza kuwa Idara yake itachukua mkakati wa makusudi kwa kushirikiana na wadau husika kuwafahamisha wananchi kuwa Mabaki ya meli zilizozama ni urithi wa Nchi na hivyo wananchi hawana haki ya kuchukua mabaki hayo bila kupata idhini ya Kitengo cha Urithi wa Mambo ya Bahari.
Akitoa historia yake Mkuu wa kitengo hicho Fakih Othman amesema kitengo hicho kilianzishwa mwaka 2011 kikiwa na malengo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufanya tafiti juu ya urithi wa baharini katika maeneo yote ya Visiwa vya Unguja na Pemba.
Malengo mengine ni pamoja na kushirikiana na taasisi mbalimbali za nje na ndani ya nchi zinazojishughulisha na uhifadhi na utunzaji wa urithi wa Baharini.
Fakih ametaja changamoto zinazokikabili kitengo cha Urithi wa Mambo ya Baharini kuwa ni pamoja na uhaba wa vifaa vya kufanyia kazi, ukosefu wa mafunzo pamoja na kutokuwepo kwa fungu maalum kwa ajili ya kuendeleza kitengo hicho.

    ZIARA YA WAZIRI WA NCHI AFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS      WA ZANZIBAR KATIKA KANISA LILILOCHOMWA MOTO

-Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar Dickson D,Kaganga akimuonesha Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohd Aboud maeneo yalioathirika zaidi baada ya Kanisa hilo kuchomwa moto katika Vurugu zilizotokea Zanzibar ambapo hadi sasa watu 30 wamekamatwa  na baadhi yao kuhusishwa na tokeo hilo.
PICHA NA YUSSUF SIMAI MAELEZO ZANZIBAR.
Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohd Aboud akielezea jambo kwa Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar Dickson D,Kaganga wakwanza kulia kuhusiana na kuchomwa moto kwa Kanisa hilo liliopo Kariakoo Mjini Zanzibar katikati ni  Mkuu wa Jeshi la Polisi I,G,P Saidi Mwemwa.
Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar Dickson D,Kaganga akielezea  kwa Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mohd Aboud na Viongozi wengine mbalimbali kile kilichotokea baada ya Kanisa hilo kuchomwa motokatika Vurugu zilizotokea Zanzibar ambapo hadi sasa watu 30 wamekamatwa  na baadhi yao kuhusishwa na tokeo hilo.
Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar Dickson D,Kaganga akibubujikwa na Machozi kwa kuguswa na hotuba iliokuwa ikitolewa na Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohd Aboud baada ya Kanisa hilo kuchomwa motokatika Vurugu zilizotokea Zanzibar ambapo hadi sasa watu 30 wamekamatwa  na baadhi yao kuhusishwa na tukio hilo.
-Mkuu wa Dini ya Kiislam Afisi ya Mufti wa Zanzibar Thabit Noman Jongo akitoa hotuba ya Dini inavyoeleza kuhusiana na kudumisha Amani na Usalama katika nchi na kuondosha mifarakano na chuki na kuharibu mali.Katika kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar ambalo limechomwa moto.
Mku wa Jeshi la Polisi I,G,P Saidi Mwema akitoa hotuba kwa Maaskofu na baadhi ya waumini wa Kikristo katika kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar lililochomwa moto,ambapo hadi sasa watu 30 wamekamatwa  na baadhi yao kuhusishwa na tokeo hilo.kuliani kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Abdalla Mwinyi na kushoto yake ni Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Mussa Ali Mussa.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar Abdalla Mwinyi Khamis akitoa hotuba na kuonyesha Umoja na Mshikamano uliokuwepo kati ya Waislam na Wakristo kwa Picha ambayo imebuniwa na Mchoraji wa kingereza na kuwataka kuendelea na mshikamano wao ili kuzidi kuleta amani nchini.
habari na fullshangwe

No comments:

Post a Comment