BABA MZAZI WA ELIZABERTH MICHAEL KIMEMETA LULU,AFUNGUKA KUHUSU MWANAE KUHUSISHWA NA SHITAKA LA MAUJI YA MSANII MWENZAKE MAREHEMU STEVEN KANUMBA.
| MICHAEL EDWARD KIMEMETA AMBAYE NI BABA MZAZI WAELIZABERTH MAARUFU KAMA LULU |
Mwigazaji wa Kike Elizaberth Micahel Kimemeta(katikati) akitoka Mahakamani jana
Baba mzazi wa Muigizaji wa kike wa filami nchini Elizabeth Michael Kimemeta maarufu kama Lulu
ambaye anahusishwa na kifo cha msanii na muandaji wa filamu nchini Steven
Kanumba amelezea kushtushwa juu ya taarifa za kifo hicho pamoja na mwanaye
kudaiwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na muigizaji huyo nguli.
Baba wa Elizabeth Michael
ambaye alijitambulisha kwa jina la Michael Edward Kimemeta(49)mzaliwa wa
Wilayni Rombo Mkoani Kilimanjaro alisema kuwa alimtambua Steven Kanumba kama mwalimu
wa mtoto wake lulu,lakini hakuamini baada ya kupata taarifa za kifo cha kanumba huku mwanae
akidaiwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Kanumba.
Msanii huyo wa kike Elizaberth Michael alifikishwa
mahakamani april 11 akikabiliwa na mashtaka ya mauaji ya msanii wa filamu
Marehemu Steven Kanumba,ikiwa ni siku nne, tangu alipokamatwa mara baada ya
kifo cha msanii huyo.
Alisema kuwa Elizaberth
Michael alizaliwa tarehe april 17/1995 hospitali ya Muhimbili jijini Dar es
Salaam ambaye alimaliza elimu ya kidato
cha nne katika shule ya sekondari ya
Midway mwaka jana na hivi sasa
anamamiaka 17.
“Umri wa Elizaberth bado
alikuwa ni mwanafunzi ukilinganisha na umri wa marehemu Kanumba na hadhi yake
katika jamii iliyodhibitishwa na mazishi yake kuhudhuriwa na umati mkubwa wa
watu”Alisema
Michael alisema kuwa ni vema polisi kuweka
uwazi katika taarifa zao za uchunguzi kwa kuzingatia kuwa tukio hilo ambalo
lilisababisha kifo cha Muigizaji Kanumba limejenga chuki na uhasama dhidi ya
msaani wa kike Lulu na ndugu,marafiki na wapenzi wa Muigizaji ambaye sasa ni
marehemu Steven Kanumba.
Alisema kuwa kilichomshtusha
zaidi ni baada ya taarifa za polisi kusema kuwa ulitokea ugomvi kati ya
Marehemu Steve Kanumba na Lulu,huku ikitajwa kuwa walikuwa wapenzi,huku akisema
kuwa Lulu alikuwa bado ni mwanafunzi baada ya kumaliza kidato cha nne mwaka
jana.
“Hatukutegemea kuwa kama Marehemu Kanumba angeweza kuwa na mahusiano na binti
yetu kwanza ndiye tuliyekuwa tukimtegemea kwa kaisi kikubwa katika kuendeleza na
kukikuza kipaji alichokuwa nacho mwanatu Elizaberth”Alisema Michael.
Alisema Upelelezi unaofanyika kuhusu kifo cha kanumba
umeegemea upande mmoja kutokana na Lulu na yeye kuwa na majeraha ya kuumizwa na
Marehemu Kanumba,na marehemu Kanumba
kudaiwa ndiye aliyeanza kumshambulia Elizaberth.
“Ninaomba Wanasheria na wanaharakati wa haki za
kibinadamu kuingilia suala hili kati na kusaidia
katika shtaka la mauaji linalomkabili mwanangu Elizaberth kwani tofauti na
linavyochukuliwa kishabiki’Alisema
Hata hivyo alisema kuwa jamii inatakiwa
kutambua mazingira ya tukio hilo,ambapo
chanzo ilitokana na ugomvi uliopelekea tafrani na Lulu kumsukuma Marehemu
Kanumba hali ambayo inaelezwa kuwa ilitokana na wivu wa kimapepenzi na
hakukusidua kumuua hivyo yeye anashangaa mwane kuhusihwa na mashtaka ya mauaji.
Alielezea chuki ambazo zilizopo kwa jamii juu ya kifo
hicho pia inatokana na jinsi viogozi mbalimbali wa nchi walivyotafsiri tukio hilo,hali ambayo pia
inachoche uhasama na badala yake wangetakiwa kuiachia mahakama kufanya kazi
yake na siyo kuhukumu kwa kusikiliza upande mmoja.
“Ushiriki wa mwanangu kuhusu mambo ya sanaa
nilikwishapata wasiwasi na mama yake mzazi akawasiliana na Marehemu Kanumba
ambaye alikuwa anamhakikisha usalama wa mwanae Lulu na kusema kuwa ataendele
kubaki kama mwalimu..lakini leo nasikia ni
mpenzi nilishtushwa”Alisema Kimemeta.
Katika hatua nyingine alitoa wito kwa wanasia,viongozi wa
dini na wanaharakati,wasomi,kuanzisha mjadala mpana utakaohusiana na uhusiano
wa Lulu na marehemu Kanumba pamoja na tukio lilisababisha kifo chake.
Hata hivyo katika
hatua nyingine Michael ameelezea kusikitishwa kwake baada ya kushindwa kuuzuria mazishi ya kumuaga
marehemu kanumba kutokana na chuki na uhasama kutoruhusu,ambayo mpaka hivi sasa
mazingira hayaruhusu,lakini pindi yatakaporuhusu hata sita kufika nyumbani kwa
marehemu Kanumba na kutoa pole.
Suala hilo la mauaji ambalo
anahusishwa lulu alisema kuwa familia haina la kufanya ila inamuachia Mungu kwa
kuwa hukumu yake ni ya haki.
Michael alisema kuwa anaungana na watanzania wote kutoa
pole kwa familia ya kanumba kutoa pole kwa msiba mkubwa ambao haukutarajiwa,na
kusema kuwa kanumba alikuwa bado ni kijana mdogo aliyeonyesha umahiri kwenye
sanaa na mpaka sasa amecha pengo kwa familia na Tanzania kwa ujumla.


No comments:
Post a Comment