Sunday, March 25, 2012




HABARI YA MKAZI WA MOSHI KUKUTWA NA MBWA ALIYEMCHUNA YAZUA GUNZO MITAANI.

PICHA YA MBWA AMBAYE ALIKUWA AMESHACHUNWA NA BWANA TOMAS TAYARI KWA KUNYWA SUPU.

Habari ya Mkazi wa Chekereni ya Kahe Wilaya ya Moshi Vijijini Thomas Mlay (28) kukutwa na mbwa aliyekuwa amemchuna imekuwa habari ambayo ilivuta hisia za watu wengi na kuwa gunzo sehemu mbambali nchini.

Tukio hilo ambalo lilitokea Machi 21 mwaka huu majira ya saa tisa mchana huko maeneo ya Chekereni ya Mabogini.Kamanda wa Polisi Absalom Mwakyoma alisema mgambo wa Kahe Chekereni alimkamata mtuhumiwa huyo akiwa amemchuna mbwa akidai kuwa anataka kula nyama yake.

Alisema kuwa mgambo huyo alipata taarifa kutoka kwa uongozi wa kijiji hicho kuwa Thomas Mlay katika hali isiyo ya kawaida akiwa nyumbani kwake aliweza kumkamata mbwa wa nyumbani kwao na kumchinja kisha kumchuna ngozi kwa nia ya kumchemsha na kunywa supu yake.

Kamanda alisema kuwa kutokana na hali hiyo wanakijiji kupitia uongozi wa kijiji cha Chekereni walimkamata na kumhoji kutokana na tukio hilo na kutoa sababu zilizompelekea kumchuna mbwa huyo kuwa ni kutaka kunywa supu yake.

Aliongeza kuwa kutokana na sababu hiyo uongozi wa kijiji walipata utata kama kweli alitaka kunywa supu kama alivyodai au alitaka kuwauzia watu kwani baada ya mbwa huyo kuchunwa alikuwa akionekana kama mbuzi mdogo.

Mwakyoma alisema uongozi wa kijiji hicho ulipata mashaka na mtu huyo na kuamua kumfikisha katika kituo cha polisi Moshi kwa mahojiano ambapo ilibainika kuwa ana matatizo ya akili. Hata hivyo, bado anaendelea kuhojiwa ili kujua kwa undani dhamira yake iliyosababisha kufanya kitendo hicho.



No comments:

Post a Comment