Sunday, March 25, 2012

Kampuni ya gesi ya Kilwa Enegy matatani

Waziri wa Nishati na Madini Willium Ngeleja.



WANANCHI wa kaya zaidi ya 3000 wa Kata  ya Kivule Wilaya Ilala wameijia juu Kampuni ya Kilwa Enegy inayotaka kuwahamisha kupisha mradi wa umeme wa gesi kwa kuchelewesha kulipa  fidia kwa zaidi ya miezi sita.

Wananchi hao wanataka tathmini  ifanyike upya  kwenye nyumba zao na walipwe fidia kwa kiwango cha kimataifa  kutoakana na kuyumba kwa uchumi  kila kukicha duniani .

Wakati kampuni hiyo ikifanya  tathmini Agosti mwaka jana  kwenye eneo la mita 60,  iliwaahidi wananchi hao itakuwa imekwisha walipa fedha zao ndani ya siku 21 kitu ambacho hakikufanyika.

Akizungumza, Mohamed Abdalraman miongoni mwa wanaobolewa nyumba zao, alisema  kutokana na ahadi hiyo, imewafanya washindwe kuendeleza maeneo yao na kusababisha baadhi ya maeneo kuwa vichaka vya majambazi.

“Hadi sasa ni zaid ya miezi sita hatujui tutalipwa lini na kiasi gani,  tunataka tathmini ifanywe upya na tulipwe kwa kiwango cha kimataifa kulingana na gharama za ujenzi zilivyopanda kwa zaidi ya asilimia 25.

“Tunaiomba Serikali  iingilie kati tatizo hili tulipwe haraka kwa sababu tumechoka kusumbuliwa na tunataka malipo yalingane na gharama za nyumba zetu ili kuepuka usumbufu, wakitulipa kidogo tutakuwa na hasira nao kila siku,”alisema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Ufuatiliaji  wa  mchakato huo, Denis Ikandilo alisema  Machi 23, mwaka huu waliwapa siku saba kampuni ya Kilwa Enegy ili iwe imetoa majibu itawalipa lipa lini. 

  Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
 

No comments:

Post a Comment