Wednesday, March 14, 2012



TALGWU KUFANYA MAANDAMANO..

CHAMA cha wafanyakazi wa serikali za mitaa Tanzania(TALGWU) Kimetishia kufanya maandamano yasiyo na kikomo iwapo serikali itapuuza ulipwaji wa haraka wa deni la zaidi ya Bil 30 ambazo ni madai ya likizo,matibabu na masomo kwa wanachama wake.

Naibu katibu mkuu wa Talgwu,Njaa Kibwana amesema deni hilo ni kwa kipindi cha zaidi ya miaka mawili iliyopita ambapo kwa sasa wanasubiri utekelezaji wa ahadi ya wizara ya Tawala za mikoa na serikali za mitaa(TAMISEMI) juu ya ulipwaji wa deni hilo.

Kibwana aliyasema hayo wakati wa mahojiano na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa semina ya siku mbili ya viongozi 75 wa wilaya wa chama hicho katika mikoa ya Arusha, Manyara, Tanga na Kilimanjaro, uliofanyika Moshi ambao waliwajengea uwezo viongozi hao.

Alisema suala la maandamano liliandaliwa kufanyika Mach 3,2012 lakini walilazimika kuahirisha baada ya maombi ya Tamisemi kwamba wanashughulikia ulipwaji wake huku mazungumzo baina ya pande hizo mbili yakiendelea.

“Ili mtu yeyote afanye kazi yake kwa ufanisi na kujituma lazima alipwe kile anachostahili kwa wakati…wanachama wetu walikwenda likizo,kupata matibabu na masomoni lakini hawajalipwa hadi sasa,tunapenda kila mtu atimize wajibu wake” alisema.

Alisema katika semina hiyo iliyoshirikisha wajumbe 75 walipewa staid za uongozi,utekelezaji wa majukumu yao,Utunzani wa fedha,Sheria za kazi,kazi za vyama vya wafanyakazi sehemu za kazi na mfuko wa hifadhi ya jamii(LAPF).

Kibwana alisema kupitia semina hiyo viongozi hao watawezesha uboreshwaji wa chama katika ngazi walizotoka ikiwamo kukumbushana masuala mapya ya uongozi yanayojitokeza ikiwamo mipango ya chama katika kuwanufaisha wanachama wake.

Hata hivyo naibu katibu mkuu alisema miongoni mwa changamoto wanazokabiliana nazo ni pamoja na uchelewashwaji wa upandishwaji wa vyeo kwa watumishi, nyongeza ya mishahara ambapo baadhi ya wafanyakazi hukumbwa na tatizo hilo kwa asilimia kubwa.

Baadhi ya viongozi walioshiriki semina hiyo wameahidi Kuleta chachu ya mabadiliko kwa wanachama huko wilayani kwani wamebaini awali walikuwa na mapungufu kadhaa ikiwamo utoaji wa taarifa mbalmbali kwa wananchma kwa wakati muafaka.

mwisho.

No comments:

Post a Comment