Sunday, March 25, 2012

              *Mbowe, amnadi Nassari
Mwenyekiti wa CHADEMA,Freeman Mbowe,akimnadi mgombea ubunge kupitia chama hicho Joshua Nassari.       


 WAKATI kampeni za uchaguzi mdogo Jimbo la Arumeru Mashariki leo zikiingia wiki ya lala salama, huku vyama viwili, Chama cha Demokrasia na Maendeleo na Chama Cha Mapinduzi vikiendelea kuumana vikali, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amewaambia watu wa jimbo hilo kuwa nchi nzima sasa inawaangalia wao hasa maamuzi watakayoyafanya ndani ya siku sita zijazo.

Akimnadi mgombea wa CHADEMA Joshua Nassar kwenye mikutano ya kampeni katika vijiji mbalimbali vya kata za Makiba, King’ori, Maroroni, Nkoarisambu na Songoro jana, Mbowe aliwaambia wananchi kuwa ‘wanazo siku saba tu za kufanya maamuzi ya msingi juu ya mstakabali wa maendeleo ya Arumeru na Tanzania kwa ujumla’ na dunia nzima inawasubiri kwa hilo.

Aliwaambia wananchi kuwa anamhitaji Nassar kwenda kuongeza idadi ya makamanda wapiganaji bungeni kwa ajili ya kuwatetea wanyonge dhidi ya watawala, hususan wakati huu ambapo nchi inajiandaa kuandika katiba mpya, ambapo aliongeza kuwa mgombea huyo ataungana na wenzake 48 kudai haki ya ardhi ziwemo ndani ya katiba mpya.

“Ndugu zangu, iko tofauti moja kubwa kati ya CHADEMA na CCM, sisi tunapigania kupata ridhaa kwa ajili kuwatetea Watanzania, kulinda rasilimali za nchi zinanufaishe wananchi wote, kupambana na ufisadi unaozidi kulimaliza taifa, lakini wenzetu tayari walishapata ridhaa hiyo, lakini wameshindwa kabisa kuitumia kwa ajili ya kusimamia rasilimali zetu kwa faida ya kizazi hiki na vizazi vijavyo.
Habari na Mwandishi wetu, Arumeru
      

No comments:

Post a Comment