Mbio za Kimataifa za Kilimanjaro Marathon zilizokuwa zikisubiriwa kwa hamu zimefanyika Leo Mjini Hapa na kushuhudia idadi kubwa ya wakimbiaji wakijitokeza kushiriki katika mbio hizo kubwa zaidi katika uknda huu wa Afrika Mashirika na Kati.
Kilimanaro Marathon
Zinazofanyika kila mwaka na Kudhaminiwa na Kampuni ya Bia ya TBL kupitia
kinywaji cha Kilimanjaro Premium Lager, mwaka huu zinafanyika tena
katika Ardhi ya Kilimanjaro ikiwa ni msimu wa 11 tangu zianzishwe.
Kwa
mujibu wa Waratibu wa Mbio hizo, Executive Solution pamoja na Wadhamini
wakuu, TBL, mwaka huu umeshuhudia wakimbiaji wapatao 6500 waliojitokeza
kukimbia katika mbio mbali mbali ukianza na Full Marathon (Km 42), Half
Marathon (Km 21), Half Marathon Disabled na Vodacom Fun Run (Km 5).
Akizungumza
katika Hafla ya kutoa Zawadi, Meneja wa Masoko ya Bia ya Kilimanjaro
Premium Lager, George Kavishe alisema kuwa umaarufu wa mbio hizo
huongezeka kila mwaka ambapo tofauti na mwaka jana ambayo ilishirikisha
wakimbiaji 6000 mwaka huu kuna ongezeko la washirki 500 na kufanya jumla
ya washiriki kufikia 6500.
No comments:
Post a Comment