Mulugo akitoa nasaha zake kwa wahitimu.
Naibu Waziri wa Elimu Nchini,Philip Mulugo amesema kuwa
Serikali inatarajia kutoa mikopo yenye dhamani ya shilingi billioni 326 katika
mwaka wa fedha 2012/2013 kwa wanafunzi wa elimu ya juu kupitia bodi ya elimu ya
juu.
Mulugo aliyasema hayo kwenye mahafali ya 5 ya chuo kikuuu
kishiriki cha Elimu Mwenge,(MWUCE)yaliyofanyika mwishoni mwa wiki,ambapo
alisema kuwa mkopo huo unatarajiwa kutolewa kwa wanafunzi wapatao 98,772.
Mahafali hayo yalihudhuriwa na wageni mbalimbali
wakiwemo,Mwenyekiti wa baraza la Chuo kikuu cha St Agustino Tanzania,John
Ndimbo,Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo kikuu kishiriki cha elimu Mwenge,Askofo Isaac
Aman pamoja na Mkuu wa chuo kishiriki cha ualimu Mwenge ,Severin Niwemugiza.
Alisema kuwa fedha hizo zitatolewa kwa awamu,ambapo mpango wa
serikali ni kuendelea kuimarisha na kuboresha usimamiaji wa utoaji wa mikopo na
urejeshwaji inayotolewa kwa wanafunzi wa elimu ya juu.
Hata hivyo alisema kuwa kuna ongezeko kubwa la wanafunzi
wanaohitimu elimu ya juu kutoka wanafunzi 14 mwaka 1964 hadi kufikia wanafunzi
166,484 kwa mwaka 2011/2012 na ongezeko la vyuo kutoka chuo kimoja hadi vyuo 42.
Alisema kuwa vyuo vya binafsi ikiwemo Mwuce vimekuwa na
mchango mkubwa katika kuleta maendelea nchi kwa kusaidia ongezeko la wataalamu
ikiwemo sekta ya Elimu.
Hata hivyo Mulugo alitoa shilingi million 10 kwa ajili ya
ununuzi wa vifaa vya mafunzo ya sayansi chuoni hapo ambavyo vilielezwa kuwa ni
changamoto kubwa kuanzisha program itakayoanza karibuni.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo kikuu kishiriki
cha elimu Mwenge,Askofu Isaac Aman alisema kuwa chuo kimekuwa kikumbana na
changamoto ya wanafunzi wanaohitimu elimu ya sekondari hususani kidato cha sita
kutokuwa na sifa stahiki ya kujiunga na chuo.
Alisema kuwa kuwepo kwa mfumo mbovu kuanzia chini wa elimu
umekuwa changamoto kubwa kwa vyuo vinavyotoa elimu ya juu,hivyo ni vema
Serikali iboreshe na kusimamia vizuri utoaji wa elimu za sekondari.
Mwisho
|
No comments:
Post a Comment