Tuesday, April 10, 2012

UZINDUZI WA KAMPENI YA KUPANDA MITI YAENDELEA MANISPAA YA MOSHI MKOANI KILIMANJARO

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjro Leonidas Gama,akizungumza wakati wa uzindizi wa kampeni ya upandaji wa miti Manispaa ya Moshi Mkoani hapa ,(katikati)ni Meya wa ,Manispaa ya Moshi Japhary Michael,na Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi Alhaji Musa Samizi
 
Hapa Mkuu wa Mkoa Leonidas Gama akizindua zoezi hilo kwa kupanda mti katika eneo lijulikanalo kwa jina maarufu la Changbuy na kuendelea kupanda katika maeneo mengine.


Mdau kutoka bank ya standard chartered akipada mti kwenye zoezi hilo la upandajiw a miti
Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi Bernadette Kinabo naye akipanda mti kwenye zoezi hilo la upandaji wa mti kwenye Manispaa ya Moshi.

Meya wa Manispaa ya Moshi Japhary Michael(Chadema)akipanda mti wake eneo la Meimorial



Wadau Mbalimbali waliohudhuria zoezi hilo la uzinduzi wa kampeni za upandaji wa mti.

Akizungumza kwenye uzunduzi wa kampeni hizo za upandaji wa miti Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama amesema kuwa zeozi hilo  litakuwa endelevu na uongozi wa mkoa utahakikisha kuwa kila miti ambayo itakuwa unaoteshwea na halmashauri zote za Mkoa wa Kilimanjar inatunzwa na kukua na siyo       kutekelezwa.

Mkuu huyo amesema kuwa katika utaratibu huo ulioanzishwa wa upandaji wa miti Mkoa wa Kili,manjaro utatarajia kupanda miti zaidi ya million 50 baada ya miaka mitano.

Amesema kuwa katika kipindi hiki cha operesheni ya upandaji wa miti wanatarajia kupanda miti zaidi ya million nane.

Amesema kuwa zoezi hilo litakuwa endelevu na ni suala la watu wote kuhakiklisha kuwa wanasimamia mazingira ipasavyo,huku akisifu wilaya za moshi Mjini na Hai katika utunzania wa  mazingira.

Alisema kuwa upandaji huo wa miti utazingatia maeneo makuu manne katika utunzaji wa mazingira kama kingo za mito,vyanzo vya maji,chemchem,milima na maeneo hayo yatatakiwa kutambuliwa na  halmashauri ili kuweza kusimamiwa ipasavyo.

"Taaisisi mbalimbali zijitokeza kusaidia halmashauri zetu ili kuweza kifanikisha mpango huu,lakini pia kwa mwaka 2013 lazima kila kijiji kuanzisha vitalu vya miti pamoja na watu binafsi na sisi tutakachofanya ni kuwasaidia upatikanaji wa miche"Alisema Gama

Hata hivyo aliwashukia wafugaji ambao wamekuwa wakiacha mifugo yao kuzagaa ovyo,huku akiwataka watendaji wa Serikali kutoza faini kubwa zaidi kwa mifugo ambayo itakamatwa ikiharibu mazingira ili kuweza kutokomeza kabisa tatizo hilo.

                                                                       

No comments:

Post a Comment