RIPOTI YA MGOMO WA WALIMU NCHINI KENYA PAMOJA NA KAULI YA SERIKALI
Ripoti
iliyoandaliwa na BBC imesema Serikali ya Kenya imekiri kwamba haiwezi
kutimiza matakwa ya walimu wa shule za misingi wanaogoma nchini humo
huku mgomo huo ukiingia siku ya tatu.
Waziri wa elimu Mutula
Kilonzo amesema wanachotaka walimu yani kuongezwa asilimia miatatu ya
mishahara yao hakiwezekani, kwa sababu pesa hizo hazikujumuishwa kwenye
makadirio ya bajeti ya mwaka huu.
Maelfu ya walimu nchini
Kenya walianza mgomo wao juzi (September 3) wakidai kuwa serikali
imekuwa ikipuuza kilio chao kuongezwa mishahara yao kwa miaka mingi
ambapo walimu hao ni wa shule za misingi na zile za upili.
Walimu hao wamekiuka agizo
la mahakama lililoharamisha mgomo huo huku shule nyingi katika miji
mikubwa kama Mombasa, Nairobi na Nakuru zilisalia kufungwa, walimu wa
shule za upili pamoja na wahadhiri wa vyuo vikuu wamesema watajiunga na
mgomo huo baadaee wiki hii ingawa tayari wameanza kususia kazi.
Mgomo huu umetokea wakati
shule zikifungua kwa muhula wa tatu kitu ambacho walimu hao wanasema
sio hoja kwani wamekuwa wakigoma kila muhula wa tatu unapofungua kwa
zaidi ya miaka kumi iliyopita wakidai hiyo nyongeza.
Wanasema kuwa serikali
haina usawa katika mishahara kwa wafanyakazi wa sekta ya umma kwani ni
hivi juzi tu wauguzi na wafanyakazi wengine wa umma waliongezwa
mishara baada ya kugoma lakini walimu wamepuuzwa.
Huu mgomo umeonekana kufanikiwa kwasababu shule nyingi zimesalia kuwa bila walimu na wanafunzi wengi wamebaki majumbani.
No comments:
Post a Comment