Tuesday, September 4, 2012

RIPOTI YA MGOMO WA WALIMU NCHINI KENYA PAMOJA NA KAULI YA SERIKALI

Ripoti iliyoandaliwa na BBC imesema Serikali ya Kenya imekiri kwamba haiwezi kutimiza matakwa ya walimu wa shule za misingi wanaogoma nchini humo huku mgomo huo ukiingia siku ya tatu. Waziri wa elimu Mutula Kilonzo amesema wanachotaka walimu yani kuongezwa asilimia miatatu ya mishahara yao hakiwezekani, kwa sababu pesa hizo hazikujumuishwa kwenye makadirio ya bajeti ya mwaka huu. Maelfu ya walimu nchini Kenya walianza mgomo wao juzi (September 3) wakidai kuwa serikali imekuwa ikipuuza kilio chao kuongezwa mishahara yao kwa miaka mingi ambapo walimu hao ni wa shule za misingi na zile za upili. Walimu hao wamekiuka agizo la mahakama lililoharamisha mgomo huo huku shule nyingi katika miji mikubwa kama Mombasa, Nairobi na Nakuru zilisalia kufungwa, walimu wa shule za upili pamoja na wahadhiri wa vyuo vikuu wamesema watajiunga na mgomo huo baadaee wiki hii ingawa tayari wameanza kususia kazi. Mgomo huu umetokea wakati shule zikifungua kwa muhula wa tatu kitu ambacho walimu hao wanasema sio hoja kwani wamekuwa wakigoma kila muhula wa tatu unapofungua kwa zaidi ya miaka kumi iliyopita wakidai hiyo nyongeza. Wanasema kuwa serikali haina usawa katika mishahara kwa wafanyakazi wa sekta ya umma kwani ni hivi juzi tu wauguzi na wafanyakazi wengine wa umma waliongezwa mishara baada ya kugoma lakini walimu wamepuuzwa. Huu mgomo umeonekana kufanikiwa kwasababu shule nyingi zimesalia kuwa bila walimu na wanafunzi wengi wamebaki majumbani.

WANAHABARI IRINGA WANUSURIKA KIFO WAKITOKA KUMZIKA MWENYEKITI WAO DUDI MWANGOSI

wanahabari ho wakijiokoa kwa kutokea mlango wa dereva baada ya gari yo kutka kupinduka huko Tukuyu Mbeya wakitoka kumzika mwenyekiti wo Daudi Mwangosi kijiji cha Busoka Tukuyu
N aibu ktibu mkuu wa IPC Francis Godwin (wa tatu kulia ) akiwa na kamati y mazishi ikiongozwa na Edo Bshir wa pili kulia
Rais wa UTPC Keneth Simbaya (kushoto) na katibu msaidizi IPC Frncis Godwin wakiongoza waombolezaji kubeba jeneza leo
Wanahabari wakisidia kulinasua gari la wnahabari lililokuwa limekwam kabla ya kutaka kupinduka wakitokea kuzika mwenyekiti wo Daudi Mwngosi,hakuna mjeruhi katika tukio hilo
                                                      Habari kwa hisani ya Francis Godwin
UMOJA WA WENYEVITI WA VITONGOJI HAI WAMTAKA RC KUFUTA KAULI KUWA ATAWAFUKUZISHA KAZI.
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wenyeviti wa Vitongoji Wilayani Hai,Saimon Mnyampanda akizungumza kwenye mkutano wao uliofanyika ukumbi wa fM Bomangombe.

Wenyeviti wa Vitongoji wakiwa kwenye umoja wao .

Wakizungumza kwenye kikao chao kilichokaa juzi kwenye ukumbi Fm bomangombe Wilayani Hai,walimtaka Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama kufuta kauli yake aliyoitoa agust 22 kwenye vyombo vya habari baada ya wenyeviti hao kugomea zoezi la kuwaongoza makarani wa sensa hadi hapo wangelipwa madai yao.

Walisema kuwa hata hivyo licha ya kukaa kikao na Mkuu wa Wilaya ya Hai Novatus makunga na kuamua kuondoa mgonmo huo,lakini hata hivyo posho zao za sensa sawa na shilingi million 5,800,000 walikuwa bado hawajalipwa pamoja na madai yao mengine ya posho ya shilingi million 280.

Walisema kuwa kauli hiyo ya Mkuu wa Mkoa ni ya Kisiasa kutokana na kutafsi sheria ya Tawala za Serikali za Mitaa ambayo inaeleza mtu mwenye mandeti ya kumuondoa madarakani Mwenyeviti wa Vitongoji ni Wananchi waliowaweka madarakani.


MHUBIRI WA KIMATAIFA KUANZA RASMI MKUTANO MKUBWA WA INJILI MOSHI.
Karibu sana Tanzania,Mhubiri wa Kimataifa Dana Morey akipokelewa na Maua baada ya kufika kwenye uwanja wa kimataifa wa Kia.

Marafiki ndugu jamaa waliokuwa wameambatana na Dana Morey.

Dana Morey akiwa na Fiance wake.

Hapa kizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali mkoani Kilimajaro


Hapa Dana Morey akipokewa na wageni mbalimbali.
 
Mhubiri wa Kimataifa kutoka nchini marekani,EvDana Morey amewataka viongozi barani afrika kuacha ubinafsi na rushwa,changamotoambazo zimekuwa zikiwakabili viongozi wengi na badala yake wafanye kazi kwauaminifu na uwazi kwa wananchi.

Mhubiri huyo aliyasema hayo wakati akizungumza nawaandishi wa habari kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kia,baada ya kufikanchini kwa ajili ya Mkutano mkubwa wa injili utakaofanyika septemba 5 hadi 9Mjini Moshi.
 
Alisema kuwa tatizo la viongozi kuwa na tamaa yarushwa pia inasababishwa na viongizi wengi kutokuwa wakweli,na kuwa na tamaa yamali,huku wakiwasahau wananchi waliowaajiri.
 
“Ujumbe wangu siyo kwa viongozi wa afrika pekeebali ni kwa viongozi wa Nchi zote pamoja na amerika kufanya kazi kwa uwazi nakwa ukaribu zaidi na wananchi waliowachagua ili kuleta maendele”Alisema Morey.
Hata hivyo aligusia suala la viongozi kufanya kazikwa umoja,na uelewa hususani ni matatizo ya wananchi,ambapo alisema kuwaviongizi wabinafsi pia wanapaswa kuwa na hofu ya Mungu,na ikiwezekana kumtegemaMungu katika majukumu yao.
Katika wakati mwingine alizungumzia suala lamapenzi ya jinsia moja(homesexual)ambapo alisema kuwa yeye na kanisa lakehawakubaliani na suala hilo,kutokana na kutompendeza Mwenyezi Mungu na piakukataza katika vitabu vyake vitakatifu.
Alisema kuwa licha ya nchi anayotoka ya Amerikakukubali ndoa hizo za jinsia mmoja lakini yeye bado ataendelea kulipinga sualahilo,pamoja na kushangaa madhehebu ambayo yatakuwa yanaunga mkono uchafu huo.


Morey ni mfanyabiashara nchini Marekani ambaye anajishughulisha na biashara ya uuzaji wa vipuri(spear)za ndege,magari na fedha anazozipata anazitumia kwenye kazi za injili kama mkutano wa injili ambao ameuandaa mjini Moshi utakaofanyika kwenye viwanja vya mashujaa.


                  HIVI NDIVYO HALI ILIVYOKUWA KWENYE MAZISHI YA  Daudi Mwangosi

 Rais wa UTPC Kenneth Simbaya akizungumza wakati wa shughuli za  mazishi ya Mwangosi.
 
Katibu mkuu wa Chadema Dk Wilbroad Silaa akizungmza mazishini. 
 Ibada ya mazishi ikiendelea.
 
  Mjane wa marehemu Mwangosi
     Mwili ukipelekwa malaloni.
    Ibada.
       Jeneza likishushwa kaburini.
     Jeneza Kaburini
  Udongo ukiwekwa kaburini
                        Mjane akilia juu ya kaburi la marehemu mumewe
                                Watoto wa marehemu wakiweka mashada
                                               Dk Slaa akieka shada la maua.
                               Rais wa UTPC Kenneth Simbaya akiweka maua.

                          Ndugu na jamaa wakiweka maua katika kaburi la marehemu Mwangosi.