Tuesday, September 4, 2012

MHUBIRI WA KIMATAIFA KUANZA RASMI MKUTANO MKUBWA WA INJILI MOSHI.
Karibu sana Tanzania,Mhubiri wa Kimataifa Dana Morey akipokelewa na Maua baada ya kufika kwenye uwanja wa kimataifa wa Kia.

Marafiki ndugu jamaa waliokuwa wameambatana na Dana Morey.

Dana Morey akiwa na Fiance wake.

Hapa kizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali mkoani Kilimajaro


Hapa Dana Morey akipokewa na wageni mbalimbali.
 
Mhubiri wa Kimataifa kutoka nchini marekani,EvDana Morey amewataka viongozi barani afrika kuacha ubinafsi na rushwa,changamotoambazo zimekuwa zikiwakabili viongozi wengi na badala yake wafanye kazi kwauaminifu na uwazi kwa wananchi.

Mhubiri huyo aliyasema hayo wakati akizungumza nawaandishi wa habari kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kia,baada ya kufikanchini kwa ajili ya Mkutano mkubwa wa injili utakaofanyika septemba 5 hadi 9Mjini Moshi.
 
Alisema kuwa tatizo la viongozi kuwa na tamaa yarushwa pia inasababishwa na viongizi wengi kutokuwa wakweli,na kuwa na tamaa yamali,huku wakiwasahau wananchi waliowaajiri.
 
“Ujumbe wangu siyo kwa viongozi wa afrika pekeebali ni kwa viongozi wa Nchi zote pamoja na amerika kufanya kazi kwa uwazi nakwa ukaribu zaidi na wananchi waliowachagua ili kuleta maendele”Alisema Morey.
Hata hivyo aligusia suala la viongozi kufanya kazikwa umoja,na uelewa hususani ni matatizo ya wananchi,ambapo alisema kuwaviongizi wabinafsi pia wanapaswa kuwa na hofu ya Mungu,na ikiwezekana kumtegemaMungu katika majukumu yao.
Katika wakati mwingine alizungumzia suala lamapenzi ya jinsia moja(homesexual)ambapo alisema kuwa yeye na kanisa lakehawakubaliani na suala hilo,kutokana na kutompendeza Mwenyezi Mungu na piakukataza katika vitabu vyake vitakatifu.
Alisema kuwa licha ya nchi anayotoka ya Amerikakukubali ndoa hizo za jinsia mmoja lakini yeye bado ataendelea kulipinga sualahilo,pamoja na kushangaa madhehebu ambayo yatakuwa yanaunga mkono uchafu huo.


Morey ni mfanyabiashara nchini Marekani ambaye anajishughulisha na biashara ya uuzaji wa vipuri(spear)za ndege,magari na fedha anazozipata anazitumia kwenye kazi za injili kama mkutano wa injili ambao ameuandaa mjini Moshi utakaofanyika kwenye viwanja vya mashujaa.


No comments:

Post a Comment