WANANCHI WALALAMIKIA ITIKADI ZA KISIASA KUGEUKA KISIKI CHA MAENDELEO.
Hapa Diwani wa Kata ya Kimochi,Anamenyisa Macha akishauri kuairishwa kwa mkutano wa wananchi baada mtendaji kushindwa kufika. |
Mwananchi akitoa hoja ya kusikitishwa kushindwa kufika kwa mtendaji huyo wa Kijiji kwenye Mkutano. |
Mkutano huo ilibidi ufunguliwe na kufungwa. |
Wananchi wa kijiji cha mdawi Kata ya Kimochi,Wilaya ya moshi
vijijini wamemlalamikia Mtendaji wa kijiji hicho Lenard Mende kwa kushindwa
kuwepo ofisi siku za kazi,pamoja na kuwa mtoro kwenye mikutano ya
Serikali,ambayo inakuwa na lengo la kujadili shughuli za maendeleo ya kijiji
hicho.
Akizungumza baada ya kufunguliwa kwa mkutano huo na
kuahirishwa bila kujadili agenda yoyote wananchi walikuwa wamefika kwenye
mkutano huo walisema kuwa hiyo ni mara ya pili kushindwa kufanyika kwa mkutano baada ya mkutano uliofanyika jula 8
mwaka huu,mtendaji huyo kuondoka baada ya kuulizwa swali na mmoja wa wananchi.
Mkti wa kijiji cha mdawi Rumisha Kinyaa aliwaeleza wananchi
waliokuwa wamefika kwenye mkutano huo ambao ulihairishwa agusti 4 mwaka huu,
kuwa walikuwa wamempa taarifa ya uwepo wa Mkutano huo Mtendaji wa Kijiji,lakini
hadi kufika muda wa mkutano hakufika.
Alisema kuwa hawataweza kuendelea na Mkutano huo,ilihali
muwakilishi wa Mkurugenzi hayupo,hivyo agenda mbalimbalimbali ambazo zingejadiliwa
kwa siku hiyo ingekuwa ni kazi bure kama wangefanya bila kuwepo kwa Mtendaji.
“Miongoni mwa mambo ambayo wananchi walikuwa wahoji kwenye
mkutano huo ni pamoja na kutokufika kwa mtendaji huyo ofisini siku za
kazi,jambo ambalo limekuwa kero kubwa kwa wananchi wa kijiji,wakati yeye
ameletwa kwa ajili ya kushirikiana na wananchi kuleta maendeleo”Alisema Kinyaa.
Kwa wake Diwani wa
Kata ya Kimochi,Anamenyisa Macha alisema kuwa changamoto nyingi zinazotokea
kwenye kijiji hicho zinatokana na itikadi za kisiasa ambazo zinasababishwa na
mvutano wa vyama vya siasa,pamoja na wananchi kupingana na kugawa kwa kijiji
cha Mdawi.
Alisema kuwa kinachotakiwa ni wananchi na viongozi kuondoa
itikadi zao na kuwatumikia wananchi,ili kuweza kuleta maendeleo,pamoja na
kuchunguza malalamiko yalipo kwa wananchi kuwa hawakuhusishwa katika ugawaji wa
kijiji hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi Ibrahim Msengi alipuulizwa kuhusiana
na tatizo lililopo kwenye kijiji hicho cha Mdawi,alisema kuwa amebanwa na
shughuli za mbio za Mwenge ambao ulikwua Mkoani Kilimanjaro,huku akiahidi
kulifuatilia baada ya kumalizika kwa mbio za Mwenge.
No comments:
Post a Comment