SERIKALI YALIFUNGIA GAZETI LA MWANAHALISI.
Serikali ya Tanzania imetangaza
kulifungia gazeti la MWANAHALISI kwa muda usiojulikana kutokana na
kuandika habari na makala za uchochezi, uhasama na uzushi likiwa na nia
ya kusababisha wananchi kukosa imani na vyombo vya dola.Taarifa iliyotumwa kwenye vyombo vya habari na ofisi ya msajili wa Magazeti Wizara ya habari, Vijana, Utamaduni na michezo imesema katika matoleo ya hivi karibuni, gazeti hilo limekua likichapicha habari na makala zenye kueneza na kujenga hofu kwa wananchi.
Taarifa imesema kabla ya uamuzi wa kulifungia Mwanahalisi, mhariri wa gazeti hilo aliitwa na kuonywa mara nyingi lakini hakuwa tayari kukiri kuwa maudhui ya makala zake hayakua na tija kwa jamii na zilikua hazifati madili ya uandishi wa habari japo amekua akinukuu kifungu cha 18 cha katiba ya Uhuru wa kutoa maoni ambapo hii ni mara ya pili kufungiwa, kabla liliwahi kufungiwa kwa miezi mitatu.
No comments:
Post a Comment