MAKUMBUSHO YA BUJORA,MOJA YA VIVUTI VILIVYOSAHAULIKA LICHA YA KUTOA FURSA YA AJIRA KWA WASANII.
Charles Madatta,kwa niaba ya Fabian Mhoja ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Makumbusho hayo akionyesha nyumba walizokuwa wakiishi enzi hizo,na wasukuma. |
Moja ya nyumba ambazo zilikuwa zikitumia na wafalme wa Kisukuma kwa ajili ya kukutana na kucheza ngoma za asili ya kisukuma. |
Makumbusho
ya tamaduni za kabila la kisukuma yaliyopo Kijiji cha Kisesa Jijini Mwanza
yameelezwa kuendelea kuwa kivutuo kikubwa afrika Mashariki na kuwavutia watalii
kutoka nchi mbalimbali za jumuiya ya Ulayana kuchangia katika
kuliingizia taifa fedha za kigeni.
Akizungumza
na blog hii,Charles Madatta,kwa niaba ya Fabian Mhoja ambaye ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Makumbusho hayo
alisema kuwa uwepo wa makumbusho hayo,licha ya kusaidia kutunza mila za
kisukuma,lakini pia yametoa ajira kwa wananchi wanaozunguka makumbusho.
Alisema
kuwa makumbusho hayo yametoa ajira kwa zaidi ya watu 100 kwenye idara mbalimbali, Miongoni mwa ajira
inayotolewa na bujora ni pamoja na wasanii wa ngoma za asili ya kisukuma kujipatia kipato kupitia sanaa yao,kwa
kualikwa ndani na nje ya nchi kama Dernmark,Marekani,Ufaransa.
Alisema
kuwa vipo vikundi vya ngoma zaidi ya 2000 ambavyo hualikwa kwa ajili ya kufanya
maonyesho ya ngoma hizo,ambapo kwa mwaka vikundi zaidi ya 30 huweza kwenda nje
ya nchi,na kutoa mchango wa kodi pamoja na wao wenyewe kunufaika na safari
hizo.
Jamii
inayozunguka makumbusho ya Bujora wanasema kuwa makumbosho hayo yameweza kuwa
mkombozi mkubwa hususani wajasiriamali wadogo wadogo,wakiwemo mama
ntilie,dereva wa bodaboda na wananchi wengine ambao hupata nafasi ya kufanya
kazi kama nlivyokwishaeleza hapo awali
.
Hata
hivyo kwa upande wa vikundi ambavyo vinacheza ngoma za kisukuma vimekuwa
vikilipwa zaidi ya 150,000 hadi 200,000 pamoja na usafiri wanapoalikwa
kutumbuiza sehemu mbalimbali za Jiji la Mwanza.
Miongoni mwa makumbusho Makumbusho
nayopatikana bujora ni pamoja na historia ya kabila la kisukuma,picha ambazo
zinaonyesha matukio ya asili,bidhaa za kazi za mikono, historia ya uchifu,
uhusiano wa kijamii, teknolojia ya uhunzi, sayansi ya uganga wa kijadi na
mifumo ya kuhesabu na majina ambayo yanafuata mfumo wa kijinsia na umri wa watu
wanaohesabu namba.
No comments:
Post a Comment