MAJAMBAZI WAPORA KITUO CHA MAFUTA NA KUTOROKA NA BUNDUKI.
JESHI la polisi mkoani Kilimanjaro linawasaka watu 10 wanaotuhumiwa kuhusika katika tukio la ujambazi lililotokea usiku wa kuamkia jana na katika kituo cha mafuta cha msaranga kilichopo katika maeneo ya mbwaruki kata ya kiboroloni, wilaya ya moshi, mkoani Kilimanjaro na kuondoka na bunduki aina ya Shot gun namba 67189.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, kaimu kamanda wa
polisi mkoani Kilimanjaro Yusuph Ilembo, alisema kwamba majambazi hao
walimvamia mlinzi wa kituo hicho aitwaye Salvatory Peter Ngowi wakiwa na
mapanga, marungu na nondo na kumjeruhi kwa kumkata kichwani usoni na mikononi
kasha kuondoka n asilaha yake aina ya shotgun pamoja na pesa za mauzo ambazo
hata hivyo kiasi chao hakijatambulika.
Kamanda Ilembo alisema kwamba baada ya kupora bunduki hiyo
ambayo ilikuwa na risasi mbili na fedha hizo majambazi hao walitokomea
kusikojulikana .
“tulipata taarifa za
ujambazi katika kituo cha mafuta cha msaranga kwamba mlinzi wa kituo hicho
amevamiwa na watu wapatao kumi, majira ya saa 2 usiku, tukio lililotokea katika
maeneo ya mbwaruki kiboroloni na tulipofika tayari majambazi hao walikuwa
wameshaondoka katika eneo la tukio na kulingana na maelezo ya mlinzi wa kituo
hicho bwana salvatory peter ngowi, watu hao walimvamia na kumpokonya bunduki
yake aina ya shotgun No.67189 ikiwa na risasi mbili pamoja na fedha za mauzo
ambazo hata hivyo idadi yake haijafahamika bado,’ alisema Ilembo.
Kutokana na kuwepo kwa matukio kama hayo katika siku za
hivi karibuni hususan katika eneo hilo la mbwaruki, kamanda Ilembo alitoa wito
kwa wafanyabiashara hasa wamiliki wa vituo vya kuuza mafuta kuhakikisha vituo
vyao vinakuwa na sehemu ya kuhifadhiia pesa iliyojengwa imara na kuongeza kama
hayo yatafanyika ikiwa ni pamoja na kuongeza umakini wawapo kazini basi matukio
kama hayo yatatokomezwa mkaoni hapo.
Aidha alisema jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro
linaendelea na msako mkali kuhakikisha watuhumiwa hao wanakamatwa na kuongeza
kuwa jeshi linatoa wito kwa wananchi kutoa ripoti maramoja kwa polisi wawaonapo watu
wanaowatilia mashaka. .
No comments:
Post a Comment