MENEJA WA SHIRIKA LA BIMA TAWI LA MOSHI MKOANI
KILIMANJARO AWATAKA WATUMISHI WA SERIKALI,WAFANYABIASHARA NA WATU BINAFSI
KUJIUNGA NA BIMA HIYO.
Meneja wa shirika la bima ya taifa tawi la Moshi Mkoani Kilimanjaro John Mdenye akizungumza na waandishi wa habari ofisi kwake. |
Waandishi wa habari(kushoto)venance Maleli wa radio moshi Fm na Gift Mongi wakimsikiliza Meneja wa Shirika la Bima ya Taifa(hayuko pichani) . |
Meneja wa shirika la
bima ya taifa tawi la Moshi Mkoani Kilimanjaro John Mdenye akifafanua jambo.
Meneja wa shirika la bima ya taifa tawi la Moshi Mkoani
Kilimanjaro John Mdenye amewataka watumishi wa Serikali,wafanyabishara na wadau
wengine kujiunga na bima hiyo huku akisema kuwa shirika hilo kwa sasa linafanya
vizuri baada ya kulipa ,madai yote ya wanachama waliokuwa wanadai kutoka Wilaya
sita za Mkoa wa Kilimanjaro.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake
Mdeye alisema kuwa malalamiko yaliyokuwepo kwa shirika hilo yalikwishafanyiwa
kazi kwa fedha za wadai kuwa tayari
lakini wakati shirika hilo zilipotembea maeneo mbalimbali hawakuweza kuonana
nao lakini wadai wote wa tangu mwaka 2009 wamekwishalipwa.
Alisema kuwa kama wapo ambao wanalalamika kuwa
hawajalipwa fedha zao zipo tayari na kinachotakiwa ni kufika kwenye shirika
hilo la bila.
Hata hivyo aliwataka Walimu wanaopenda mkopo
kwenye taasisi za fedha za kijamii kujiunga na bima hiyo kutokana na utofauti
mkubwa uliopo baina taasisi hizo za kifedha
za kijamii shirika hilo la bima ya taifa.
Alisema mwenendo wa shirika hilo kwa sasa ni
mzuri tofauti na miaka 1996 ambapo alieleza changamoto zilizokuwepo kwa kipindi
hicho kuwa ni pamoja na soko huru (liberalization) na kuchangia kuwepo kwa ushidnani
mkubwa kwa taasisi binafsi zilizojihusisha na na utoaji huduma wa bila.
“Hali ya shirika la Bima ni nzuri kwasasa na tangu mwaka 2009 shuka chini hakuna madai yoyote
na kama yapo basi ni wale waliohama maeneo au kushindwa kufika kuchukua madai
yao ambapo Meneja huyo aliwataka kufika kwenye shirika hilo ili kuchukua madai
yao”Alisema Mdenye.
Alibainisha kuwa zaidi
ya shilingi billion 935 zimeweza kulipa
madai yaliyokuwepo kwa wadai na kubainisha kuwa miaka ya 2009 kurudi
nyuma madai hayo yalichangiwa na shirika kukabiliwa na changamoto ya
kuwepo kwa maradhi mengi ikiwemo UKIMWI
ambayo yalichangia kuwepo kwa vifo vingi.
Kwa upande wa mawakala wanaojishughulisha na
masuala ya bima ambao wamekuwa wakisababisha usumbufu mkubwa kwa wateja alisema
mawakala hao wanawajibu wa kuwaelimisha wateja umuhimu wa kujiunga pamoja na
huduma mbalimbali za bima,lakini kama watakuwa wanafanya kinyume wakibainika
watachukua hatua za kisheria.
No comments:
Post a Comment