MAHAKAMA KANDA KUU YA ARUSHA YAMVUA UBUNGE GODBLESS LEMA LEO.
![]() |
Godbless Lema. |
Mahakama kanda Kanda kuu ya arusha leo imemvua Ubunge aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema kwa tiketi ya CHADEMA.
Uamuzi huo umefikiwa Aprili 5, 2012 mbele ya Jaji Mfawidhi wa Kanda ya Sumbawanga, Gabriel Rwakibarila katika hukumu ya kesi ya kupinga matokeo ya Ubunge Jimbo la Arusha hilo yaliyo wasilishwa na wanachama watatu wa CCM waliotaka Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kutengua ushindi
wa Mbunge huyo.
Wana CCM hao waliofungua kesi hiyo ni pamoja na Mussa Mkanga (55), Happy Kivuyo (49) na Agnes Molle (44).
Wanachama hao wanadai kuwa taratibu za maadili ya uchaguzi zilikiukwa wa kuwa mshindi alitumia lugha za kashfa, matusi na kejeli katika mikutano ya kampeni aliyofanya jimboni Arusha.
Katika kesi hiyo wadai walileta mashahidi 14 kwenda kutoa ushahidi wao katika mahakama hiyo na wadaiwa walifanikiwa kuwaleta mashahidi 5 kujitetea.
Kuvuliwa Ubunge kwa Lema, kuna kuja siku chache wakati bado cha hicho kipo katika shamra shamra za ushindi wa Ubunge jimbo la Arumeru Mashariki mkoani humo.
No comments:
Post a Comment