Mwalimu akiwa kazini(Picha kwa hisani ya maktaba) |
Baadhi ya waalimu wa shele za sekondari wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, wametishia kugoma kufundisha na wengine kutaka kuacha kazi, kutokana na mishahara yao kukatwa shilingi elfu 90 kila mwezi bila maelezo yeyote ya msingi.
Wakizungumza na blog hii ya www.tanzania-leo.blogsport.com, Waalimu hao ambao baadhi yao hawakutaka majina yao yaandikwe, walisema kuwa mishahara yao imekuwa kikatwa kiasi hicho cha fedha kwanzia mwezi wa kwanza mwaka huu hadi sasa bila sababu yeyote.
Walisema kuwa licha ya wao kudai malimbikizo ya nyuma, wameshangazwa na kitendo cha kukatwa tena mishaara yao bila kupewa taarifa yeyote, hali waliyodai kuwa kiwango kidogo kinachobaki wanashindwa kukidhi mahitaji yao ya msingi, ukilinganisha na garama za maisha zilivyo juu.
“Sisi hatutakuwa tayari keendelea kuingia madarasani huku mishaara yetu ikizidi kuchukuliwa kinyemela, kila mwezi kukatwa elfu 90 ni pesa nyingi sana kwa maisha yetu sisi waalimu...tunataka tupewe maelezo ya msingi kwanini fedha hizo zinakatwa” walisema waalimu hao.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake Kamishina wa Serikali za Vyuo Vikuu Kanda ya Kaskazini, Bernad Adam alisema kwa hawatakuwa tayari kuendelea kufanya kazi ambayo inakandamiza haki za waalimu.
Adamu alisemakuwa tamko hilo limetokana na wao kudai malimbikizo ya muda mrefu, lakini wakati huo huo wanakatwa tena mishahara yao kwa kiwango kikubwa bila sababu zozote.
Alisema kuwa endapo viongozi wa serikali hawatachukulia swala hilo hatua za msingi kutokana na tatizo hilo kuwa kubwa na kero kwa waalimu, linaweza kuleta matatizo makubwa kwa kupelekea waalimu
kugoma na wengine kuacha kazi.
Naye katibu wa Chama cha waalimu wilaya ya Hai (CWT), Dawson Temu alikiri kuwapo kwa tatizo hilo na kueleza kuwa katika mikutano yake amekuwa akiwasihi waalimu kuandika barua lakini tangu mwezi Januari
hadi sasa hakuna hatua zozote zilizotekelezwa.

Temu alisema kuwa tatizo limeonekana kuwa Idara kuu na hazina kwani barua zimeandikwa na mkurugenzi mtendaji wilaya amewajibika kulishughulikia lakini imeonekana kukwama ngazi za juu.
Kwa upande wa M kurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Hai Melzedeck Humbe, alikiri kuwapo kwa malalamiko hayo na kueleza kuwa tatizo hilo limetokana na mfumo wa kisasa wa ulipaji mishaara .
Alisemakuwa tatizo hilo limewakumba watumishi zaidi ya 200 wakiwemo watumishi wa halmashauri hiyo, na kusema kuwa hayo ni makosa madogo madogo hutokea wakati wa malipo huko hazina.
Mkurugenzi huyo aliwataka watumishi wote na waalimu waliokatwa mishaara yao kupeleka barua zilizoidhinisha mishaara yao kwa lengo la kushughulikia tatizo hilo hazina, ili fedha hizo ziweze kurejeshwa na
kueleza kuwa hakuna mwalimu aliyeshushwa daraja na kupunguziwa mshaara.

No comments:
Post a Comment