Sunday, April 28, 2013

SAKATA LA MACHINGA KUTII KAULI YA MBUNGE MSIGWA , LACHUKUA SURA MPYA IRINGA

polisi Iringa  wakiwa katika  eneo la Mashine tatu ,kuondoa mawe na magogo ambayo yalitumika  kuziba barabara hiyo kama  sehemu ya  kushinikiza  serikali  kuwaruhusu kuendelea  kufanya kazi ya umachinga  eneo hilo  lisiloruhusiwa
Kamati ya  ulinzi na usalama ya wilaya ya Iringa ikiwa  imekutana mchana  huu kwa  kikao cha dharula  kufuatia Machinga  kutekeleza kauli ya mbunge Msigwa  ya kuvunja sheria
Hii  ndio hali halisi  iliyopo  eneo la mashine tatu baada ya machinga  kurejea  eneo hilo leo



KAULI mbunge wa jimbo hilo Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) kuwataka wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) kurejea kufanya kazi katika eneo la barabara ya Mashine tatu
nusuru asababishe machafuko makubwa eneo hilo kati ya  polisi na Machinga.
 
Msigwa ambae aliitoa kauli hiyo mwanzoni mwa  wiki  iliyopita  katika mkutano wa wabunge wa chadema waliosimamishwa bungeni ,mkutano uliofanyika katika uwanja wa Mwembetogwa mjini hapa,kwa kuwataka Machinga kurejea eneo hilo na iwapo mtu atafika kuwanyanyasa basi wana----!!!?
Machinga hao jana wameitikia kauli hiyo kwa kurejea eneo hilo na kupelekea askari wa kutuliza ghasia (FFU) kutanda eneo hilo na kushindwa kutumia nguvu zaidi ya kuwataka wafanyabiashara hao kuendelea na shughuli zao eneo hilo .
Wakizungumza na mwandishi  wa habari hizi eneo la tukio  wafanyabiashara hao  walisema  kuwa  wamelazimika  kurejea  katika  eneo  hilo baada ya mbunge  wao Mchungaji Msigwa  kuwaruhusu  kufanya biashara katika  eneo hilo ambalo mwanzoni  walihamishwa na kupelekwa Mlandege .
Hivyo  walisema  ilikuwa ni  vigumu kwao kuondolewa na  polisi katika  eneo hilo ambalo mbunge kama mwakilishi  wao bungeni na vikao  vya baraza la madiwani amewaruhusu .
“ujue  tulianza  kuwashangaa sana polisi wa FFU kufika katika  eneo hili na mabomu ya machozi kutaka kutotoa  wakati wao wenyewe  walikuwepo katika mkutano  wa Chadema pale mwembetogwa ambapo mbunge wetu Msigwa alituruhusu kurejea  eneo hili….kweli  tungeshindwa kulielewa jeshi la  polisi iwapo  wangetumia nguvu kutuondoa  sisi  wakati aliyetoa kauli ya  kuturuhusu anafahamika “
 
Kwa  upande  wake mwanasheria  wa Halmashauri  ya Manispaa ya Iringa, Innocent Kihaga alisema  kuwa eneo hilo kisheria limepigwa marufuku kwa  biashara  za umachinga na  kuwa kwa mtu ambae atapatikana akifanya biashara hapo faini yake ni shilingi 50,000 ama kifungo cha miezi sita jela ama vyote kwa pamoja.
Hatua  hiyo ya machinga  kurejea  katika  eneo hilo la barabara imeonyesha  kuichanganya  serikali ya  mkoa  wa Iringa na  kulazimika  kukutana kwa masaa kadhaa na kamati ya  ulinzi na usalama.
 
Akizungumzia suala  hilo mwenyekiti  wa kamati ya  ulinzi na usalama ya wilaya ya Iringa na kaimu mkuu  wa  mkoa  wa Iringa Dr Leticia Warioba ambae ni mkuu  wa wilaya ya Iringa  alisema  kuwa serikali  ya mkoa  inapinga kwa  nguvu zote kitendo cha wafanyabiashara hao kurejea  eneo hilo.
Dr Warioba alisema  kuwa anashangazwa na hatua ya  mbunge  Msigwa  kuwaruhusu  wafanyabiashara hao  kuvunja sheria  wakati mbunge  huyo katika  vikao  vya baraza la madiwani katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ni diwani ni katika maamuzi ya  kuwatoa wafanyabiashara  hao alishiriki .
 
Hata  hivyo Dr Warioba  aliwataka wafanyabiashara  hao kwa  jumapili  ijayo  kutofanyabiashara  eneo hilo na kuonya  wale  wote watakaokiuka kauli  hiyo na sheria iliyowekwa  juu ya kutofanya biashara  katika maeneo yasiyo rasmi.
Wakati huo mbunge wa jimbo la Mbeya mjini ,Joseph Mbilinyi (MR SUGU) jana  ameonekana katika Manispaa ya Iringa akiingia katika mashine ya kutoa pesa ATM ya NMB iliyopo nje ya jengo hilo la Manispaa ya Iringa na kusalimiana na viongozi wa Manispaa waliokuwepo nje ya jengo hilo.
BREAKING NEWS...IRINGA SI SHWARI MVUTANO KATI YA MACHINGA NA POLISI WATISHIA USALAMA

Machinga wakiendelea na  shughuli zao kama kawaida  eneo la mashine  Tatu asubuhi  hii kutokana na kauli  ya mbunge Msigwa kuwaruhusu kurejea ,chini polisi  wakiwa eneo hilo

Hali  si  shwari katika Manispaa ya Iringa baada ya kauli   mbunge  wa  jimbo hilo Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) kuwataka wafanyabiashara  wadogop wadogo (machinga) kurejea kufanya kazi katika eneo la barabara  ya Mashine  tatu kutekelezwa na machinga  hao.
Msigwa ambae  aliitoa kauli hiyo April 23 mwaka  huu katika mkutano wa wabunge wa chadema  waliosimamishwa  bungeni ,mkutano  uliofanyika katika  uwanja  wa Mwembetogwa  mjini hapa,kwa  kuwataka Machinga  kurejea  eneo hilo na iwapo mtu atafika  kuwanyanyasa  basi wana----!!!?
Machinga  hao  leo  wameitikia kauli  hiyo kwa  kurejea  eneo hilo na kupelekea askari  wa  kutuliza ghasia (FFU) kutanda  eneo hilo na kushindwa  kutumia nguvu  zaidi ya  kuwataka wafanyaiashara hao  kuendelea na shughuli  zao  eneo hilo .
habari na francis godwin.Iringa.

No comments:

Post a Comment