Thursday, April 18, 2013

KITIMA "DEMOKRASIA YA TANZANIA IMETEKWA NA WATU WACHACHE"

Makamu mkuu wa chuo Kikuu cha St Augustine Dr Charles Kitima Akisisitiza jambo wakati akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari,hawapo pichani.




Na Rodrick Mushi,Mwanza.

, amesema kuwa demokrasia ya Tanzania imetekwa na watu wachache,huku kukiwepo na msukumo mkubwa kutoka chama tawal (CCM),kuendelea kukandamiza demokrasia ya vyama vingi ili kiendelee kubaki madarakani.

Kitima aliyasema hayo mwishoni mwa wiki, wakati akifunga mafunzo kwa waandishi wa habari za uchunguzi za biashara kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini yaliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Best Ac, jukwaa la kilomo(ANSAF)kwa kushirikiana na  chuo kikuu cha St Augustino Mwanza.

Mbali na kuwepo kwa matukio mbalimbali ya ukandamizaji wa demokrasia  Kitima alisema kuwa muda wa CCM kuondoka madarakani ukifika wataondoka kwa aibu na wataingiza taifa kwenye mahafa mabaya mbeleni.

“CCM ni chama kizuri na sera zake ni nzuri ila kinaponzwa na watu wachache, mwisho wa siku wananchi wataikataa kwa kutoleta mabadiliko pamoja na kutotaka kuondoka madrakani”Alisema Kitima.

Alisema kuwa nchi ya Tanzania ingepaswa kuongozwa kwa nchi za afrika mashariki kuwa nchi yenye demokrasia bora,kutokana na misingi aliyoacha baba wa Taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere lakini misingi hiyo imepotoshwa na baadhi ya viongozi waliokosa uadilifu.

Kitima anasema  kuwa demokrasia ni kujali utu na kuheshimu haki ya kila mtu,watu kujitawala na kuweka serikali inayowajibika kwao,na pindi itakashindwa kuwajibika itapaswa iondoke na kuomba msamaha kwa kushindwa kuwatendea haki wanananchi walioichagua.

“Inasikitisha nchi yenye demokrasia na mfumo wa vyama vingi kusikia chama tawala kikijidai majukwaani kuwa kitaendelea kutawala milele,wakati wananchi ndiyo wenye maamuzi ya mwisho,huo unaweza ukawa ni ukiukwaji wa demokrasia au kujiendesha kidikteta”Alisema Kitima.

Kutokana na matukio ya kutekwa kwa demokrasia Kitima alisema kuwa hali hiyo inaendelea kulelewa nchini,na kuendelea kukua kwani mtu ambaye anaweza kuiba kura kwenye uchaguzi au kugaramikia wizi wa kura anapewa cheo na kudhaminiwa.

Matukio mengine ya ukiukwaji wa demokrasia aliyoelezea Kitima ni pamoja na kufunguliwa kwa kesi wabunge wa upinzani zaidi ya 10 kwa wakati mmoja,na kushinda kuwatumikia wananchi,huku akihoji ni kwa nini hakuna Mbunge wa chama tawala ambaye amekuwa akifunguliwa kesi kama wanavyofanyiwa wa upinzani?

Hata hivyo alieleza kuwa kwa nchi yenye Demokrasia wananchi wanapaswa kua na sheria zao,ikiwa ni pamoja na haki ya kuwawajibisha viongozi waliowachagua kwa kushindwa kuwajibika kwao.

Alisema kuwa Mwalimu Nyerere alijenga misingi mizuri ya demokrasia nchini ya watu kuheshimiana na kuheshimu haki za wengine,lakini misingi hiyo imeachwa na baadhi ya viongozi wa sasa.

“Wakati wa enzi za Mwalimu Nyerere michezo hiyo haikuwepo na alikuwa akigundua unataka kuteka demokrasia kwa kuwanyima haki wananchi usingeweza kupata madaraka kama inavyofanyika hivi sasa”Alisema Kitima.

Mwisho

No comments:

Post a Comment