Sunday, April 28, 2013

CHADEMA KUMSHITAKI MKUU WA MKOA WA ARUSHA MAGESA MULONGO.


CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo mkoa wa Arusha(CHADEMA)kimesema kuwakinatarajia kumfungulia mashitaka mkuu wa mkoa wa Arusha MagesaMulongo dhidi ya kauli zake za uchochezi  dhidi ya Chama hicho  lakinipia kauli za vitisho kwa Mbunge Lema ambaye kwa sasa anashikiliwa naPolisi.
Akizungumza na vyombo vya habari mapema jana Katibu wa chama hichoAmani Golugwa alisema kuwa zoezi hilo lipo mbioni kukamilika kwa kuwawanasheria wa chama hicho tayari wameshapewa taarifa hizo
Golugwa alisema kuwa Magesa Mulongo amekuwa kikwazo kikubwa sana kwakuwa sio mara ya kwanza kutoa lugha za uchochezi dhidi ya Chademalakini hata mara nyingine amekuwa akimtuhu Lema kwa uongo uongo haliambayo hadi kwenye mauaji ya chuo cha uasibu ilijitokeza
Aliendele akwa kusema kuwa kama wataweza kupuuzia hali hiyo itazidikuwaumiza sana na ikubambikiwa kesi ambazo si za kwao kama hali ilivyokwa sasa ambapo kuna dalili za Mbunge Lema kubambiwa kesi ya mauajiyaliyotokea katiika chuo cha Uasibu
“tunavyoongea mpaka sasa tayari tumeshawasiliana na wenzetu ambao niwanasheria wa Chadema na tutamfikisha mahakamani huyu Mkuu ili iwefundisho kubwa sana manake kauli zake za uchochezi na za kutupingasisi zinatuchosha sana na mimi kama Katibu naona amefilisika kisera nahata kimawazo kwa kuwa kamwe siwezi mfananisha hata na mtendaji wanguwa chama”aliongeza Golugwa
Akiongelea Kesi inayomkabili Mbunge Lema alisema kuwa mpaka sasamlalamikaji katika kesi hiyo hakuna lakini vitisho alivyotoa mkuu huyowa mkoa vinasema kuwa Lema kwa sasa hatabanduka na wala hatachomokahali ambayo ni fedheha tu lakini wao kupitia kwa mwanasheria waowanajopanga vilivyo kukabiliana na Mkuu huyo wa mkoa
Awali Wakili wa Mbunge Lema ambaye ni Bw Humprey Mtui alisema kuwaanashangazwa na kitendo cha jeshi la polisi kumvunjia hesima mbungeLema na badala yake kumfanya kama Kapurwa mtaani kwa shinikizo lamaslahi ya watu wacheche
Alisema kuwa kwa mujibu wa sheria Lema angepswa kuitwa na Polisilakini kama angetaa basi ndio angeweza kuchukuliwa sheria kama hiyolakini sio kwa kitendo cha polisi walichokifanya cha kuvuka ukuta wanyumba ya mbunge huyo
Bw Mtui alisema kuwa mbali na hayo pia hata haki za msingi kama vilekuswaki na kunywa chai mbunge huyo ananyimwa na Polisi jambo ambalo niukiukaji mkubwa sana wa Sheria ya Maabusu hapa Nchini ukilinganishakuwa yeye bado ni mbunge na tena mwakilishi wa wananchi
Alifafanua kuwa bado watakuwa na mbunge huyo na wataweza kufuatasheria za msingi lakinii kwa wale wote ambao wanamuonea Mbunge huyowatachukuliwa sheria ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani kwanihali za uoneaji dhdi yake zinaongezeka siku hadi siku.

No comments:

Post a Comment