Sunday, June 3, 2012

MKUU WA MKOA WA ARUSHA NA WABUNGE WAOBWA KUCHANGIA TIMU YA FLAMINGO

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo.

 MKUU wa mkoa wa Arusha, wabunge wa mkoa huo na wadau wengine wa michezo, wameombwa kuikoa timu ya Flamingo  ambao ni mabingwa wa soka mkoa huo, kutojiandoa katika mashindano ligi ya kanda kituo cha Mara kutokana na ukata.


Wakizungumza na Libeneke la kaskazini kwa simu, viongozi wa timu hiyo inayoongoza katika kundi lake, iliyopo kituo cha mkoani Mara, kushiriki ligi ya Kanda, walisema kama wasipopata msaada wa haraka wanaweza kujiondoa katika ligi kuu kwani hawana hata fedha za chakula na kulipia vyumba vya kulala.

Katibu mkuu wa Timu hiyo, Shabani Juma  na Meneja wa timu hiyo,khatibu Ally walisema licha ya timu hiyo, kuongoza katika kundi lake kutokana na kujikusanyia alama tano lakini wanakabiliwa na ukata.

"tunaomba Mkuu wa mkoa, wabunge wetu wa mkoa wa Arusha na wadau wengine watusaidie fedha walau za chakula na kulala tu"alisema Juma.

Alisema kwa ambao wanaweza kuwasaidia wanaweza kuwatumia fedha kwa kutumia Mpesa namba 075660440 ya Katibu wa timu Shambani Juma au tigo pesa namba 0719420112 ya Meneja Khatibu Ally.

Naye Ally alisema bado wachezaji wote wa timu hiyo na viongozi, wamepania kuhakikisha wanaongoza ligi katika kituo hicho na hivyo kupata nafasi ya kupanda daraja.

Timu hiyo ya Flamingo, hadi sasa imejikusanyia poiti tano, baada ya kuifunga timu ya Ashanti magoli 2-1, mabingwa wa mkoa Kilimanjaro Forest FC walitoka nao sale sambamba na timu wenyeji Polisi Mara juzi.

Flamingo ni timu ambayo imeanzishwa na vijana wa eneo la Olmatejoo katika jiji la Arusha na imekuwa ni moja ya timu bora mkoani Arusha kwa zaidi ya miaka mitatu sasa lakini ukata umekuwa ukiikwamisha kupanda daraja.

No comments:

Post a Comment