UCHAGUZI UFARANSA MAMBO YAMEIVA SARKORZY ASHINDWA KWENYE UCHAGUZI.
Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha kisoshalisti nchini Ufaransa Francois Hollande, ameshinda duru ya kwanza ya uchaguzi nchini humo.
Kura nyingi zikiwa zimehesabiwa Bw
Hollande tayari amepata asilimia 28 ya kura.
Nicolas Sarkozy anafuatia kwa asilimia 27 hii ikiwa ni
idadi ndogo zaidi kwa rais yoyote wa taifa hilo ambaye amewahi kugombea tena kiti hicho.
Haijawahi kutokea kuwa rais aliyemadarakani anashindwa
kwenye duru ya kwanza ya uchaguzi.
Na matokeo haya yanampa mpinzani wa Rais Sarkorzy,
Francois Hollande nafasi nzuri sana
katika duru ya pili ya uchaguzi huo utakaofanyika baada ya wiki mbili.
Hata hivyo kilicho washangaza wengi baada ya matokeo hayo
kutangazwa ni idadi ya kura chama kinacho egemea upande wa kulia kilipata.
Kwa makadirio tu, mtu mmoja kati ya wapiga kura watano
nchini Ufaransa alikipigia kura chama hicho, hii ikiwa idadi kubwa zaidi ya
kura chama hicho cha Front Nationale kilicho pata kwenye uchaguzi wowote nchini
humo.
Rais Sarkorzy anasema matokeo hayo yanaonyesha hali ya
wasi wasi raia wa nchi hiyo wanayo na ni kura ya maoni dhidi ya utawala wake.
Hata hivyo ametoa changamoto kwa mpinzani wake ajitokeze
kwenye mdahalo kati yao
kabla duru ya pili ya uchaguzi huo.
Lakini bila shaka kutokana na uchache wa kura alizopata
dhidi ya Rais Sarkorzy, kiongozi huyo wa chama cha kisoshalisti, Francoise
Hollande atakuwa makini sana
asipoteze kura muhimu.
Bw Hollande anasema wafaransa wanaimani na mradi wake kwa
nchi hiyo ambao umelenga kurejesha haki, usimamizi bora wa uchumi wa nchi,
ukuzaji wa nafasi za kazi, kulinda viwanda na kujiandaa vyema kwa siku za usoni.
SOURCE BBC.
No comments:
Post a Comment