Monday, April 23, 2012

LULU APANDISHWA KIZIMABANI KWA MARA YA PILI MAHAKAMA YA KISUTU 

Mwigizaji wa Sinema Ezeckiel Michael aliyevaaa nguo nyekundu akiwa ameambatana na askari magereza alipopandishwa kwa mara ya pili kizimbani kusikilizwa kwa shauri linalomkabili kwenye Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam



Hali ilikuwa hivi Ezeckiel Michael aliambatana na askari mbalimbali wa Magereza ambao walikuwa wanamlinda asipata ghazabu kutoka kwa watu mbalimbali waliokuwa mahakamni hapo.
                                                                                
Hapa akiwa ameambata na askari wa Kike.



Gari la Magereza lililomleta Lulu na kumrudisha Magereza hadi hapo Mei 7 kesi hiyo itakaposikilizwa tena.
Askari waliokuwa wameizunguka mahakama ya Kisutu wakiwa wamevalia mikanda iliyojaa mabomu

 

Kamishna wa tume za haki za binadamu Joacquine De-Mello leo amejitokeza katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu akiambatana na Mawakili wengine wa kujitegemea kumtetea msanii wa sinema Elizaberth Michael maarufu kama Lulu.

Akilitaja jopo la Mawakili wanaomtetea lulu wakili wa kujitegemea Kenedy Fungamtama alisema kuwa mama De Mello ni miongoni ,mwa mawakili pamoja na Furgence Massawe na Peter Kibatala hata hivyo hawakuongea mahakamani hapo.

Wakili wa Serikali Elizaberth Kaganda alidai kuwa kesi imekuha kutajwa hata hivyo upelelezi haujakamilika na kuomba tarehe nyingine kutajwa na kupangwa kutajwa Mei 7.

Hali ilikuwa tofauti ba ilicvyotarajiwa Lulu leo alikuwa katika huzuni wa hali ya juu huku askari magereza wakiwa wamevalia mikanda  yenye mabomu ya machozi ikiwa ni katika kukabilia na rapsha ya aina yeyote ambayo ingeweza kutokea .

Kitu kingine ni kwamba msanii huyo alifika akiwa amevalia gauni refu na mtandio wake mwekundu walitu walijaa lakini siyo kwa wingi ambao wengi walitarajia kutokana na umaarufu alio nao Lulu hata kabla ya kufikwa na tuhuma  hizo za kesi ya mauaji ya aliyekuwa Msanii nyota wa Filamu nchini Steven Charles Kanumba.

No comments:

Post a Comment