CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI ARUSHA(AJTC) CHAFANYA MAHAFALI YAKE YA NNE. |
Viongozi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji(AJTC)wakiwa pamoja na Mgeni Rasmi wa tatu kutoka kushoto,
ambaye ni mwanahabari
Mkongwe nchini na mkufunzi kutoka shirika la utangazaji la Uingereza Joseph
Msami,wa pili kutoka kushoto ni Mkurigenzi wa mafunzo wa Chuo hicho Joseph Mayagilla.
|
\Wahitimu wakiimba wimbo kwa huzuni mbele ya wagenu na wanafunzi wanaobaki chuoni(hawapo pichani) |
Mkurugenzi wa Mafunzo Joseph Mayagille akiwatoa neno kwa wahitimu. |
Mgeni Rasmi Joseph Msami akitoa Nasaha zake kwa Wahitimu |
WAKAGUZI CREW WAKIWA KAZINI |
BURUDANI MBALIMBALI ZILIKUWEPO,HAWA NI WANACHUO WENYE VIPAJI VYA PEKEE AMBAO WANATAMBULIKA KAMA INTERNET ARMY. CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI ARUSHA(AJTC) CHAFANYA MAHAFALI YAKE YA NNE.
Chuo cha uandishi wa habari na
utangazaji cha Arusha (AJTC) kimefanya mahafali yake ya nne kwa wahitimu wa
ngazi ya cheti na Diploma ambapo wahitimu wapatao 70 wa ngazi ya cheti
walitunukiwa vyeti pamoja na 7 wa ngazi ya diploma.
Mahafali hayo yalifanyika kwenye
ukumbi wa PPS uliopo jijini Arusha,ambapo mgeni rasmi kwenye mahafali hayo
alikuwa ni mwanahabari Mkongwe nchini na
mkufunzi kutoka shirika la utangazaji la Uingereza Joseph Msami.
Kwenye mahafali hayo wanafunzi waliomaliza
mafunzo ya ngazi ya Cheti Samweli Dida na Jackline
Joel ambao walifanya vizuri walipata nafasi ya kuendelea na masomo yao ya diploma bure,kwa
mujibu wa vigezo vilivyowekwa na chuo.
Lakini pia sio tu kwa wanafunzi wa
ngazi ya cheti waliopata nafasi ya masomo bure pia waliomaliza diploma na kufanya vizuri,akiwemo
Onesmo Mbise,Jackline Heriel na Prisca Mnzava walipata nafasi ya kufanya kazi
kwenye chuo hicho,ambao watapewa mafunzo ya miezi mitatu kabla ya kuanza kazi.
Mkurugenzi wa mafunzo wa chuo cha
Arusha Joseph Mayagille alisema wapo wanafunzi wenye uwezo ila waliochaguliwa wana uwezo mkubwa na kuona ni
bora kuwabakisha chuoni hapo kwa kusaidia kuwapika wanahabari wapya na wao
kujipatia ajira.
Kutokana na tatizo la ajira
alisema kuwa chuo hicho kimekwisha anzisha utaratibu wa kutoa mafunzo ya
ujasiriamali,ili kuwawezesha wahitimu kuibua miradi na kuwa na vipato.
Kwa upande wake Mgeni rasmi kwenye
mahafali hayo,Msami alisema kuwa wahitimu hao wanakabiliwa na changamoto
mbalimbali ikiwemo kuweza kufanikiwa malengo yao waliojiwekea na kuepuka kujiingiza kwenye
matendo maovu yanayoweza kuwa chanzo cha kushindwa kufikia malengo.
Alisema kuna tatizo kubwa la
wanafunzi wa vyuo kutajwa na taasisi mbalimbali kuwa vimekuwa vikiongozwa kwa
wanafunzi kuwa na maambuzi ya Ugonjwa wa UKIMWI,jambo ambalo ni hatari kwa
taifa na maendeleo ya mwanachuo mwenyewe.
Habari na picha zimewekwa na Rodrick Mushi wa Blog ya Tanzania leo.
|
No comments:
Post a Comment