MWENYEKITI WA CCM ANGOLEWA MADARAKANI NA WANANCHI.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Hai akizungumza kwenye mkutano na wananchi wa kijiji cha kwasadala. |
Mwenyekiti aliyengolewa madarakani Erenest Samwel akijitetea baada ya kusoma kwa tuhuma zilizokuwa zinamkabili. |
Wananchi wakifuatilia kwa makini mkutano wa kumuondoa madarakani mwenyekiwa wa kijiji |
rodrick mushi.
Mgogoro uliokuwa umedumu kwa muda mrefu baina
ya Mwenyekiti wa kijiji cha Kwa sadala Erenest Samwel (CCM) na wananchi,jana
ulifikia kikomo baada ya kufanyika kwa mkutano mkuu na wananchi kumkataa
mwenyekiti kuendelea kubaki madarakani kwa kupiga kura za kutokuwa na imani
naye.
Mkutano huo ulilazimishwa kufanyika na
wananchi baada ya uongozi uliokuwa umetoka Wilayani kutaka kuhairisha mkutano
huo wa kupiga kura za kutokuwa na imani na Mwenyekiti kwa madai ya akidi
haijatimia kitu ambacho wananchi walikipingana nacho.
Baada ya mzozo wa hapa na pale hatimaye
wananchi na uongizi Uongozi wa Wilaya kupitia kwa katibu tawala Mpotwa walikubalina kupigwa kwa kura za kutokuwa na imani
naye ambapo malalamiko ya Mwenyekiti yalisomwa na kutakiwa kuyatolea ufafanuzi
kabla ya kufanyika kwa zoezo la kura za abaki madarakani au aondoke.
Mmoja wa wananchi
akizungumza kwenye mkutano huo Haji Mwasha alimtaka Katibu tawala aliyefika
kwenye kijiji hicho,kutoa fursa ya mawazo na mamuuzi ya wananchi kusikilizwa na
kufanyiwa kazi ili kuondoa dhana ambayo mwenyekiti amekuwa akiwatisha wananchi
kuwa ameshawahonga viongozi wa Wilaya.
Wananchi wakionekana kuwa na jazba kwa madai ya
matendo ya mwenyekiti,kura 154 ziliweza kumkataa kutoendelea na uongozi,huku kura
125 zikikubali aendelee kubaki madarakani hivyo kwa matokeo hayo kumfanya mwenyekiti kukosa
sifa ya kuendelea kuongoza.
Diwani wa Kata ya Masama Kusini Issa
Kisanga,alisema kuwa miongoni mwa tuhuma zilizomuondoa mwenyekiti huyo
madarakani ni pamoja na kuuza maeneo ya wazi kiholela,kuingiza kijiji kwenye
mgogoro na kanisa,kutoa lugha chafu kwenye Mikutano ya hadhara,pamoja na
kutofanya mikutano ya kusoma mapato na matumizi.
Alisema baada ya hatua hiyo kufikiwa
kilichobaki ni wananchi kusubiri uongozi wa Wilaya kutangaza taratibu za kumpata mwenyekiti wa
kijiji wa muda kwa ajili ya kuongoza kijiji huku kukisubiriwa kutangazwa kwa
uchaguzi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji hicho
aliyevuliwa uongozi Erenest Samwel alipopewa nafasi ya kujibu tuhuma mbalimbali
alizokuwa anatuhumiwa nazo na wananchi,alipinga baadhi ya malalamiko kama ya
uuzaji wa maeneo,huku akisema kuwa malalamiko mengine ni ya kupandikizwa.
Mwisho
No comments:
Post a Comment