UMOJA WA MATAIFA WATOA BILL 11KUWEZESHA KIWANDA CHA MADAWA ARUSHA.
Umoja
wa nchi za Ulaya umetoa kiasi cha Sh bilioni 11 kwa ajili ya
kukiwezesha kiwanda ch kutengeneza madawa ya binadamu cha TPI
kilichopo njiro Mkoani Arusha, ambapo kitaanza kutengeneza dawa za kurefusha maisha kwa waathirika kwa ugonjwa wa ukimwi .
Hayo
yalisemwa na Balozi wa Nchi za Umoja wa Ulaya, Timoth Clarke wakati
alipokuwa akielezea nchi za umoja wa ulaya zinavyojitahidi kutoa
misaada mbalimbali ya kimaendeleo hususan katika sekta ya afya, elimu
,vifo vya kinamama na watoto .
Alisema
katika kiwanda hicho kumeanzishwa kitengo cha kutengeneza dawa za
kurefusha maisha kwa waathirika wa VVU na kwamba kiwanda hicho kama
hakitafunguliwa ,Taifa linaweza kupoteza nguvu kazi ambazo zinatokana
na wale wagonjwa waliokumbwa na maambukizi hayo na kuongeza kuwa
kupatikana kwa dawa hizo nchini kutawezesha wale walioathirika na
ugonjwa huo kuendelea na shughuli mbalimbali za kijamii ambazo zinaweza
kuinua uchumi wan chi.
Alisema si busara kwa nchi kuwatenga waathirika wa ukimwi sehemu mbalimbali bali jamii inatakiwa kuwapa TANZANIA
ni nchi mojawapo inayojitahidi kutokomeza maambukizi ya Virusi vya
Ukimwi kwa kutumia kampeni mbalimbali ikiwemo kupunguza vifo vya
kinamama na watoto vinavyotokana na ugonjwa huo.
No comments:
Post a Comment